Yanga na Simba waliwezaje kuwashawishi watanzania hadi wakawa wapinzan wakuu katika soka hapa Tanzania?

School fiz

Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
42
Reaction score
36
Kama wewe n mfatiliaji mzuri wa mpira wa miguu utakubaliana na mimi kwamba timu tajwa hapo juu ndio znaongoza kwa mashabik hapa tanzania....tupeane mawazo ilikuaje wao tu na hakuna upinzan mwingine uliotokea hapa tanzania katika mpira wa miguu kwa wanaume
 
Muzungu aliacha hivyo, kila kitu unachokiona hapa alianzisha Muzungu, sisi hakuna kitu tunaweza, hata tu maana ya football club hatuielewi ndo maana unaona mtu anaishi Bongo anakwambia yeye mtu wa FC Barcelona au anaishi Kigoma anakwambia yeye mwanachama wa Simba FC ya Dar wakati Kigoma kwao kuna timu!
 
hizo timu zina majina mazuri tuu na sio nje ya hapo, ni sawa na ambaye ametoka huko madongokuinama akafika dar akisikia coco beach atatamani atoke kwao chamazi mpaka coco kwa miguu.
 
Muzungu aliacha hivyo, kila kitu unachokiona hapa alianzisha Muzungu, sisi hakuna kitu tunaweza, hata tu maana ya football club hatuielewi ndo maana unaona mtu anaishi Bongo anakwambia yeye mtu wa FC Barcelona au anaishi Kigoma anakwambia yeye mwanachama wa Simba FC ya Dar wakati Kigoma kwao kuna timu!
We na we hebu acha uongo na uache kujitungia maswali. Sasa swali ni kwanini kuna upinzani wewe unaleta stori za wazungu mara Barcelona mara Football Club na komedi kibao.

Timu za mpira kua pinzani huchagizwa na yafuatayo.

-Kufuatana muda kwa hizo timu kuanzishwa kwake mfano Simba na Yanga.

-Kutokea eneo moja mfano Arsenal na Totenham

-Mmoja kua kinara kwa ubingwa mfano Arsenal na Manchester United na Chelsea.

Hizo ni sababu kuu na ninadhani Simba na Yanga zinafit kote. Sasa wewe Barbra unaleta stori za mzungu daah acha kua mbaguzi aisee.
 
Unafahamu kitu kinaitwa derby? mfano Real madrid vs Atletico madrid
Arsenal vs Chelsea
Everton vs Liverpool

Hizo ni mechi ambazo kila timu huwa inajaribu kuonesha kwamba wao ndio magwiji wa sehemu husika na mara nyingi zinakua mechi ngumu sana.
Kikubwa kilichochangia ni huo "uderby" na kwa wakati huo ndio timu zilizokua zinafanya vema hivo kuchochea huu ushindani.
 
Mbona ndo zile zile sababu zenyewe za kuipenda CCM na Chadema.
 
Muzungu aliacha hivyo, kila kitu unachokiona hapa alianzisha Muzungu, sisi hakuna kitu tunaweza, hata tu maana ya football club hatuielewi ndo maana unaona mtu anaishi Bongo anakwambia yeye mtu wa FC Barcelona au anaishi Kigoma anakwambia yeye mwanachama wa Simba FC ya Dar wakati Kigoma kwao kuna timu!
Yaani ww unajifanya unawachukia rangi nyeupe, wakati iyo ITEL unayotumia wametengeneza wao
 
Unafahamu kitu kinaitwa derby? mfano Real madrid vs Atletico madrid
Arsenal vs Chelsea
Everton vs Liverpool

Hizo ni mechi ambazo kila timu huwa inajaribu kuonesha kwamba wao ndio magwiji wa sehemu husika na mara nyingi zinakua mechi ngumu sana.
Kikubwa kilichochangia ni huo "uderby" na kwa wakati huo ndio timu zilizokua zinafanya vema hivo kuchochea huu ushindani.

Mpenzi wa Everton anaishi mahali ambapo hiyo timu inatoka au mpenzi wa sijui Manchester anaishi Manchester pia, huwezi kukuta Muzungu anaishi mji au nchi nyingine akawa mpenzi wa timu ktk sehemu nyingine, hiyo ndo maana ya football club, ni club!

Hivyo kwa mfano kama wewe unaishi Mwanza haupaswi kuwa Mwanachama wa Yanga/Simba au sijui Manchester, hilo lipo Afrika tu kwa maana hatuelewi maana ya football club!
 
Kuwepo muda wote kwenye ligi katika level ya juu ya kiushindani.

Ziliwahi kuwepo timu kama Sigara, Pan Africa, Pamba nk ambapo kama zingepata uwekezaji wa moja kwa moja zingeweza kuwa na washabiki pia.

Mfano Azam, imeanza kupata washabiki sasa hivi, kama itadumu itapata washabiki.
 
Mpenzi wa Everton anaishi mahali ambapo hiyo timu inatoka au mpenzi wa sijui Manchester anaishi Manchester pia, huwezi kukuta Muzungu anaishi mji au nchi nyingine akawa mpenzi wa timu ktk sehemu nyingine, hiyo ndo maana ya football club, ni club!

Hivyo kwa mfano kama wewe unaishi Mwanza haupaswi kuwa Mwanachama wa Yanga/Simba au sijui Manchester, hilo lipo Afrika tu kwa maana hatuelewi maana ya football club!

Kwa hiyo pale Manchester wapenzi wa mpira wamegawanyika vipi katika kusapoti man city na man u? Manake mji mmoja unaweza kuwa na timu zaidi ya mbili, pale Madrid kuna Atletico na Real.

Umewahi kusikia fanbase ya timu katika nchi nyingine? Mfano arsenal wana fanbase yao Marekani, ndio maana hata kipindi cha maandalizi ya msimu wanafanya tour ili kuongeza fanbase yao.

Sidhani kama soka ni hobby yako, we endelea na CCM vs CDM mkuu, it suits you better.
 
Muzungu aliacha hivyo, kila kitu unachokiona hapa alianzisha Muzungu, sisi hakuna kitu tunaweza, hata tu maana ya football club hatuielewi ndo maana unaona mtu anaishi Bongo anakwambia yeye mtu wa FC Barcelona au anaishi Kigoma anakwambia yeye mwanachama wa Simba FC ya Dar wakati Kigoma kwao kuna timu!
Hakuna Simba FC kuna Simba SC
 
Kwa hiyo pale Manchester wapenzi wa mpira wamegawanyika vipi katika kusapoti man city na man u? Manake mji mmoja unaweza kuwa na timu zaidi ya mbili, pale Madrid kuna Atletico na Real.

Umewahi kusikia fanbase ya timu katika nchi nyingine? Mfano arsenal wana fanbase yao Marekani, ndio maana hata kipindi cha maandalizi ya msimu wanafanya tour ili kuongeza fanbase yao.

Sidhani kama soka ni hobby yako, we endelea na CCM vs CDM mkuu, it suits you better.

Huwezi kukuta Muzungu anatoka na anaishi labda mji wa Liverpool akawa mpenzi wa labda Chelsea au huwezi kukuta mtu anatoka Barcelona akawa mpenzi wa timu ya Madrid, ndiyo maana ikaitwa football club, Afrika mko hivyo kwa maana hamuelewi maana ya football club, mnaunga tela tu kama yalivyo mambo mengi bila ya kuelewa!
 
Back
Top Bottom