Yanga na Ushirikina:Mliberia afichua Maji ya Kichawi, Mrwanda ayanywa


Mkuu bado yale yale ya stori za migahawani
Leta Ushahidi
Mambo ya Yanga tumewawekea ushahidi...hadi wa picha
 

Mkuu usihangaike sana, records zimeandikwa klabu ya Simba ilipigwa faini mwaka Jana kwa kuendekeza mno matendo ya kishirikina viwanjani.
 
Toa ushahidi mkuu...kuongea tu kwa hearsay kila mtu anaweza.....huo uzi uliotuelekeza utaukimbia mwenyewe tu hata usiwe na haraka

Let exhibits speak themselves.
 

Attachments

  • Simba1.jpg
    10.2 KB · Views: 128
  • Simba2.jpg
    9.6 KB · Views: 123
  • Simba3.png
    38.7 KB · Views: 280
  • Simba4.png
    24.8 KB · Views: 109
  • Simba5.png
    32.9 KB · Views: 120
  • Okwi 1Uchawii.jpg
    44.5 KB · Views: 109
  • Okwi 2 Uchawii.jpg
    41.4 KB · Views: 108
  • Okwi 3 Uchawii.jpg
    48.8 KB · Views: 98
Let exhibits speak themselves.


Mkuu umeweka picha nyingi unfortunately hizo picha za hapo watu hapo juu wenye kuku hatuoni sura zao....Nani anaweza kujua kuwa ni simba? kwa sababu tu wamevaa nguo nyekundu? mbona Coastal pia wanavaa?

Hilo jeneza ni ushabiki wa kawaida tu...kama wewe unadhania huo ni ushirikina basi tatizo liko kwako unayedhania
 
Kwani ile timu iliyotishia kuuhama uwanja wa ccm kirumba kule mwanza kwa madai kuwa wanalogwa na timu ya toto africa na kusababisha kupoteza michezo mitatu mfululizo sio ya ligi kuu!!!!?
Na ile iliyomvua mtu bukta uwanjani kule Tanga kwa imani za kishirikina na hata baada ya kumdhalilisha mjeda wa watu bado litimu lao likachezea kichapo ilikuwa ni ya daraja la ngapi vile?
 
Mkuu usihangaike sana, records zimeandikwa klabu ya Simba ilipigwa faini mwaka Jana kwa kuendekeza mno matendo ya kishirikina viwanjani.
Msimu huu ni nani aliyepigwa faini alipokwenda Shinyanga kwa kuruka ukuta wa uwanja kisa imani za kishirikina?
 
Kidogo Cannavaro anajitahidi kufikiri japo na yeye bado hayupo sawasawa. Hivi Yanga mnashindwa kweli kufikiri japo kidogo kama punje moja ya vumbi kweli! Hivi kama kweli uchawi ungekuwa dili katika soka Timu za Mikoa ya Rukwa, Katavi na Bagamoyo (Pwani) zingekuwa hapo zilipo kweli?
 

Mkuu Freeland nakushukuru kwa mawazo yako ukijaribu kuibua shaka (maana huhitaji ku-prove your innocence), naomba twende pamoja kwenye picha ya chini ambapo kuna maneno 'Mganga afunguka nyota Simba, Yanga wanavyoroga makaburini' baada ya maneno hayo kulia kuna picha ndogo 2 (picha hizo ni zile zile zinazoonekana mwishoni mwa mstari wa kwanza, picha ya 3 na ya 4 kutoka kushoto, picha hizi ni mwendelezo wa picha ya 1 na ya 2); ya kwanza kuna mtu ameshikilia mpira na mwingine kaning'niza kuku, ya pili kuna watu wawili wameshikilia kitu kilichofunikwa. Naomba uzitazame kwa umakini picha hizo kisha linganisha na yale maneno niliyonukuu hapo juu.

Maneno yametaja Simba, Yanga (yakimaanisha Simba na Yanga wote ni washirikina, hakuna Coastal Union wala Nyota Nyekundu hapo): Kwa ushahidi wa picha hizo hakuna shaka yoyote kuwa klabu iliyokuwa inawanga ni Simba.

Kwa upande mwingine, nashukuru kwa kuwa umetambua kwamba jeneza la Okwi (akiwa Yanga) haukuwa ushirikina isipokuwa kwa yule anayedhania hivyo. Kauli hii hii itumike pia kwa vitendo vya kuchukua gloves, taulo au hata maji ya kunywa si ushirikina isipokuwa kwa yule anayedhani hivyo.
 

Kwetu sisi tunajua gloves, taulo au hata maji ni vitu vya kawaida tu...ni ninyi mliosema kuwa mlikua mnashindwa kufunga kwa sababu timu pinzani aidha kipa ana taulo golini,ana maji au gloves...its you guys who said that....Hizo picha zako hazishawishi kwa sababu hazina evidence ya watu wanaofahamika kama ni simba...nguo nyekundu sio sababu kwa sababu hata Yanga mnaweza kuvaa nguo nyekundu mkajifanya simba na mkafanya vitendo hivyo kwa sababu ni kawaida yenu.

Mfano halisi ni kabla ya mechi ya jana ...tangu timu imeenda Tanga imekuwa ikilala makaburini....na kukwepa kufanya mazoezi uwanja wa mkwakwani
 
kwanini Yanga wanaamini ktk ushirikina? ndio maana timu haiendelei kamwe asilani
Siisemei Yanga, ila naomba kuweka sawa mambo 4. (1) Kuna tofauti baina ya ushirikina na kuamini uchawi. Ushirikina ni kuabudu asiyekuwa Mwenye enzi Mungu, uchawi ni kuamini ama kuogopa nguvu za giza au chochote kisichoeleweka. Timu zetu zinaangukia kwenye hili la pili. Ila haziko peke yao kwenye hilo, kwa hivyo ni ujinga, ushamba na upuuzi kuzibeza timu zetu tu huku tukitukuza wengine wafanyao zaidi ya hayo, kwa sababu tu si Watanzania wala Waafrika. (2) kitendo chochote kinachoipa timu ama mchezaji kujiamini kwenye mchezo wake ni msaada kwa mchezaji na timu hiyo. Muhimu tu kisipingane na ustaarabu, sheria, kanuni na taratibu zetu na za kimpira. (3) Kwa nini wastaarabu wanaolaani ushirikina wa Yanga wasijiulize zaidi mambo rahisi ya msingi: (a) kwa mechi ya Mapinduzi Cup dhidi ya Shaba, je ni kawaida golikipa kubaki na glovu za akiba chini ya goli, hasa ndani ya nyavu? Si vifaa vyote vya akiba vinabaki na wachezaji wa akiba kwenye dawati la ufundi? Marefa ilikuwaje wasilione hilo? (b) Kwa mechi ya Ndanda, ni kawaida golikipa kubaki na chupa ya maji akiwa golini? Na kama ni kwa matumizi yake, kwa nini ayasokomeke nyuma ya nyavu ambako hata kuyafikia ni taabu kwake? (4) Hivi kuondoa glovu ama maji hayo inakuwa ni jambo kubwa kuliko yafuatayo? (a) Michael Jordan alikuwa ni lazima avae kaptura yake ya Chuo Kikuu cha Carlifonia ndani ya bukta ya timu kwenye kila mechi ya Chicago Bulls, jambo lililomlazimisha kuvaa bukta kubwa zaidi kuliko kawaida. Hatimaye bukta hizo kubwa ukawa ndio mtindo wa NBA nzima. (b) kabla ya kila msimu wa Wimbledon, Bjorn Borg aliwacha kunyoa ndevu zake. Akaishia kutwaa taji hilo mfululizo 1976 - 1980. (c) Serena Williams amezoea kuenda na malapa yake ya msalani hadi kwenye uwanja anaochezea mashindano, ni lazima adunde mpira mara 5 kabla ya 'serve' yake ya kwanza na mara 2 kwa 'serve' ya pili. (d)Kolo Toure lazima awe wa mwisho kuingia uwanjani kwenye mechi yoyote. Mechi ya fainali ya Ulaya dhidi ya AC Roma aligoma kuingia mwanzoni mwa kipindi cha pili hadi Gallas aliyekuwa akitibiwa alipoingia. Toure akalimwa kadi ya njano alipoingia baada ya hapo. (e) John Terry kwenye kila mechi huegesha gari yake mahali hapohapo, anatumia vikinga ugoko hivyohivyo kwa miaka 10 mfululizo mpaka vilipopotea kwenye mechi ya ugenini dhidi ya Barcelona. (f) laurent Blanc alikuwa akibusu upara wa golikipa wake Barthez kabla ya kila mechi ya Kombe la Dunia 1998. (g) wakati mmoja Pele alimvulia jezi shabiki mmoja baada ya mechi. Mechi zilizofuata kiwango chake kikaonekana kupungua, mpaka alipomwomba rafiki yake kuifuatilia jezi hiyo. Baada ya hapo mambo yakajipa tena, ingawa kuna habari kwamba jezi aliyorejeshewa haikuwa ileile. (h) Kipa Sergio Goycochea wa Argentina alikuwa akikojoa kiwanjani kila ulipofikia wakati wa penalti tanotano. Akaitoa Yugoslavia kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia 1990, akaitoa na Italia kwenye nusu fainali. Wakazitoa Columbia na Brazil kwenye kombe la Marekani Kusini 1993. (i) Rais wa klabu ya Piza alikuwa akimwaga chumvi kabla ya kila mechi ya mashindano kiwanjani kwao, dhidi ya watani wao wakubwa wa Cesena alimwaga kilo 26 nzima. Na kadhalika. Na kadhalika. Kwa nini iwe nongwa kufanyika hapa kwetu tu, tena madogo kuliko hayo? Acheni hizo!
 


Bro una matatizo makubwa sana
Wewe ni mchawi na wewe ni mshirikina
 
Bro una matatizo makubwa sana
Wewe ni mchawi na wewe ni mshirikina
Inawezekana, kwa mujibu wa vigezo vyako. Maana yake ni kwamba ili uweze kunitathmini hivyo, wewe ni zaidi ya mimi kwenye yote mawili mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…