Pre GE2025 Yanga Princess Mabingwa wa Samia Women’s Super Cup 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Yanga Princess wameibuka mabingwa wa Samia Women’s Super Cup 2025 baada ya kuichapa JKT Queens 3-0 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa katika Uwanja wa Aga Khan.

IMG_3405.jpeg
Timu hiyo ilionesha ubora wake tangu hatua za awali, ikitinga fainali kwa ushindi mnono wa 7-0 dhidi ya Fountain Gate Princess katika nusu fainali. JKT Queens, kwa upande wake, iliichapa Simba Queens 1-0 kufuzu fainali.

Soma, Pia: Ligi Kuu ya Wanawake yasimamishwa kupisha Samia Women Super Cup

Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu ilitangulia fainali hiyo, huku Simba Queens na Fountain Gate Princess zikipambana kuwania nafasi hiyo ambapo Simba Queens wamemaliza nafasi ya tatu katika michuano ya Samia Women’s Super Cup

IMG_3406.jpeg
 
Ni habari njema, angalau timu imeanza kuimarika na kuonesha ushindani katikati ya hao Giants wawili JKT Queens na Simba Queens. Bado kwenye ligi sasa wanatakiwa kutoa upinzani halisi angalau wawe kwenye nafasi za juu na kunyakua ubingwa maana kwa kumbukumbu zangu sidhani kama Yanga Princess imewahi kuchukua ubingwa toka kuanzishwa kwa ligi ya wanawake., JKT&Simba wamechukua mara 4 kila mmoja Yanga Princess bado. All in all, hongera kocha wa mpira Edna Lema Mourinho, lakini pia kwa viongozi wa Yanga wanaosimamia hii timu kwakweli kwa msimu huu wamefanya usajili mzuri.
 
Kabisa, motisha kubwa sana kwao Yanga Princess ambao wako kwenye project ya kujenga timu bora na yenye kushindania mataji
 
Haya mambo tunalazimishwa tu, timu za wanaume bado tunamtegemea GSM, halafu fungu la kuendesha timu za wanawake litoke wapi?

Binafsi siungi mkono soka la wanawake, wao mchezo wao ni netball ungeimarishwa mchezo huo.
 
Ni habari njema, angalau timu imeanza kuimarika na kuonesha ushindani katikati ya hao Giants wawili JKT Queens na Simba Queens. Bado kwenye ligi sasa wanatakiwa kutoa upinzani halisi angalau wawe kwenye nafasi za juu na kunyakua ubingwa maana kwa kumbukumbu zangu sidhani kama Yanga Princess imewahi kuchukua ubingwa toka kuanzishwa kwa ligi ya wanawake., JKT&Simba wamechukua mara 4 kila mmoja Yanga Princess bado. All in all, hongera kocha wa mpira Edna Lema Mourinho, lakini pia kwa viongozi wa Yanga wanaosimamia hii timu kwakweli kwa msimu huu wamefanya usajili mzuri.
Umeandika vema kabisa
Sasa wahamishie nguvu kwenye ligi msimu ujao washindanie kombe
 
Ni habari njema, angalau timu imeanza kuimarika na kuonesha ushindani katikati ya hao Giants wawili JKT Queens na Simba Queens. Bado kwenye ligi sasa wanatakiwa kutoa upinzani halisi angalau wawe kwenye nafasi za juu na kunyakua ubingwa maana kwa kumbukumbu zangu sidhani kama Yanga Princess imewahi kuchukua ubingwa toka kuanzishwa kwa ligi ya wanawake., JKT&Simba wamechukua mara 4 kila mmoja Yanga Princess bado. All in all, hongera kocha wa mpira Edna Lema Mourinho, lakini pia kwa viongozi wa Yanga wanaosimamia hii timu kwakweli kwa msimu huu wamefanya usajili mzuri.
Umeandika vema kabisa
Sasa wahamishie nguvu kwenye ligi msimu ujao washindanie
Kama wamewafunga JKT wametisha
Sana maana JKt kwa soka la wanawake ni habari nyingine wale kina Stumai ni tishio
 
Yanga Princess wameibuka mabingwa wa Samia Women’s Super Cup 2025 baada ya kuichapa JKT Queens 3-0 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa katika Uwanja wa Aga Khan.

Timu hiyo ilionesha ubora wake tangu hatua za awali, ikitinga fainali kwa ushindi mnono wa 7-0 dhidi ya Fountain Gate Princess katika nusu fainali. JKT Queens, kwa upande wake, iliichapa Simba Queens 1-0 kufuzu fainali.

Soma, Pia: Ligi Kuu ya Wanawake yasimamishwa kupisha Samia Women Super Cup

Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu ilitangulia fainali hiyo, huku Simba Queens na Fountain Gate Princess zikipambana kuwania nafasi hiyo ambapo Simba Queens wamemaliza nafasi ya tatu katika michuano ya Samia Women’s Super Cup

Kama kulikuwa na kombe basi ni wazi mbinu zile zile zilizozoeleka kwa wakiume zimetumika.
Huo ubora wameutoa wapi ghafla hivi?

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Ni habari njema, angalau timu imeanza kuimarika na kuonesha ushindani katikati ya hao Giants wawili JKT Queens na Simba Queens. Bado kwenye ligi sasa wanatakiwa kutoa upinzani halisi angalau wawe kwenye nafasi za juu na kunyakua ubingwa maana kwa kumbukumbu zangu sidhani kama Yanga Princess imewahi kuchukua ubingwa toka kuanzishwa kwa ligi ya wanawake., JKT&Simba wamechukua mara 4 kila mmoja Yanga Princess bado. All in all, hongera kocha wa mpira Edna Lema Mourinho, lakini pia kwa viongozi wa Yanga wanaosimamia hii timu kwakweli kwa msimu huu wamefanya usajili mzuri.
Kwenye ligi wapo nafasi ya saba
 
Eti uto wa kike wanamfunga JKT 3-0, we umesikia wapiii?
 
Haya mambo tunalazimishwa tu, timu za wanaume bado tunamtegemea GSM, halafu fungu la kuendesha timu za wanawake litoke wapi?

Binafsi siungi mkono soka la wanawake, wao mchezo wao ni netball ungeimarishwa mchezo huo.
Mzee wangu Matola Selemani Sele acha ujinga
 
Back
Top Bottom