Simba 3-0 hadi Sasa, yaani hawa Yanga princess wanacheza Kama kikundi cha wahuni tu uwanjani Kama walivyo Kaka zao kina Sarpong.
Hawa wadada wa Simba wanacheza mpira mzuri saana, kiukweli soka la wanawake limebadilika sana kwa wanao tazama huu mchezo basi wanapata burudani ya kutosha kabisa.
Ball control ipo juu, wadada wapo imara hawaanguki ovyo Kama vile vituko tulivyo vizoea hapa ni tofauti kabisa, wanapiga pasi zinafika, wanakimbia na mipira vizuri sana.
Kubwa zaidi nimependa sana jinsi walivyo na nguvu za miguu wanapiga mashuti hawa wadada balaa, makombora wanayo piga huwezi amini Kama limetoka kwenye mguu wa mwanamke.
Hongera kwa kocha Mussa H Mgosi kazi yako nimeiona.