Mimi si shabiki wa hizi timu mbili za Kariakoo, lakini niwe fair, mashabiki wa Simba wa JF Wana tatizo kubwa la uelewa ukimwondoa NAWATAFUNA. Ni huyu pekee unaweza kubishana naye masuala ya soka ukapata kitu. OKWI BOBAN SUNZU alikuwa vizuri awali, siku hizi sijui karogwa na kina Scars wasiojua chochote basi naye kawa kama shabiki maandazi. SALGANO naye ni kajipoteza kwenye kundi la Wahuni. GENTAMYCINE namhifadhi kutokana na mahusiano yaliyopo Kati yangu na yeye na tuna mkataba wa kutosemana Kwa lolote. Mshana Jr anabaki katika orodha ya wanaojua nini wanafanya, yeye na Shadeeya ni mashabiki hasa.