Yanga SC bado sana

Yanga SC bado sana

Ndiyo upuuzi wa GSM,alianza kuwekeza kwenye vyombo vya habari kuipamba Yanga akafeli sasa amewekeza kwenye hujuma ili wachezaji wa Simba waumizwe akiamini itampa ubingwa. Huyu anachoweza ni kukwepa kulipa kodi tu.
Anachoweza GSM ni kumfunga kolo tu
 

Attachments

  • VID-20211004-WA0009.mp4
    7.4 MB
Kama mikia ilivoteswa na dodoma jiji Hadi kupewa kadi ndo mshinde.kalale kolokolo
Muda Ni mwalimu mzuri na muda una tabia ya kuadhibu bila huruma.

Utopolo wekeni akiba ya maneno, ndiyo KWANZA ligi imeanza.
 
Yanga na Simba kila mmoja kacheza mechi 2,Tofauti ni kwamba Yanga ana point 6 na Magoli 2 wakati Simba ana point 4 na Goli 1.

Bado Simba mnaangaika kuifutilia Yanga wakati huo huo ushindi wa Simba ni wa kupewa pewa mechi ya kwanza alipewa penati dakika za mwisho ili kuhokoa jahazi ikashindikana mchezo wa jana mchezaji wa Dodoma jiji akala Nyekundu ili kuwadhoofisha Dodoma jiji ndiyo unaona kocha wa

Simba anafanya mabadiliko na kuingiza mafowadi tegemezi wote Boko,Kagere,Mugalu hali bado ikawa ngumu na mpira wao wa Butu Butu hakuna tena Biriani wanakuja kupata goli kwenye dakika ya 70 huko yani vululu vululu pamoja na Dodoma jiji kuwa pungufu kwa zaidi ya dakika 50 bado Simba alikuwa anacheza hovyo hovyo Sasa acha hiyo nenda kaangalie shot on Target hazifiki 3 na hata utengenezaji wa nafasibza Magoli hakuna kitu yani ni hovyo hovyo.

Bado wanajitia moyo na kuichambua Yanga wao wanajiona wako sawa. Mechi ya Yanga dhidi ya Geita Gold Yanga kanyimwa goli la Mayele mtaalamu wa kufunga yule yule aliyewaua Simba goli la wazi limekataliwa wala halikuwa Offside wachambuzi wote wanalizungumzia na hata hivyo Yanga walitengeneza nafasi kumi na moja za kufunga Magoli ukiachana na Magoli mawili yaliyokataliwa kwa kisingizio Cha Offside .

Nenda kwa Simba Angalia mechi zao uchezaji wao na utengenezaji wa nafasi za Magoli hakuna kitu.Nawaambia Simba ni suala la Muda tu wajue wanaenda kutia aibu klabu Bingwa tena watakula kipigo Cha kuwaaibisha na ndipo mtajua kweli timu yenu iko hovyo kwa Sasa bado mnajifanya hamuelewi ila mtaelewa tu siku si nyingi.

Msimu huu ni giza Totoro kwa Simba wale mashabiki lialia mjiandae kupokea matokeo ya hovyo/ matokeo tia maji tia maji/Matokeo vululu vululu.
Kadi Nyekundu ndiyo utakuwa msaada wenu vinginevyo hakuna kitu
Hivi zile story za UNBEATEN ziliishia wapi mwaka jana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ndiyo upuuzi wa GSM,alianza kuwekeza kwenye vyombo vya habari kuipamba Yanga akafeli sasa amewekeza kwenye hujuma ili wachezaji wa Simba waumizwe akiamini itampa ubingwa. Huyu anachoweza ni kukwepa kulipa kodi tu.
Hivi wewe,unajua nguvu ya hamasa na Propaganda kwenye Jambo lolote? Pamoja na mambo mengine Taasisi au mtu yoyote akifanikiwa kuwekeza kwenye hamasa na Propaganda lazima afanikiwe.
 
Hivi wewe,unajua nguvu ya hamasa na Propaganda kwenye Jambo lolote? Pamoja na mambo mengine Taasisi au mtu yoyote akifanikiwa kuwekeza kwenye hamasa na Propaganda lazima afanikiwe.
Sasa mbona Utopolo haijafanikiwa? Pamoja na mbeleko tuliyowatupia kushiriki CAF CL wameishia kulifedhehesha Taifa kwa kupigwa nje ndani
 
Back
Top Bottom