Yanga SC imebeba jukumu la kuvunja utawala huu CAF

Yanga SC imebeba jukumu la kuvunja utawala huu CAF

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259
IKIWA Juni 3, 2023 inatarajiwa kuchezwa mechi ya mkondo wa pili wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, wawakilishi wa Tanzania, Yanga SC wana kazi moja kubwa ya kuweka historia na kuvunja utawala ulioweka kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Kumbuka Yanga SC watakuwa uwanjani nchini Algeria kucheza dhidi ya USM Alger baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa Mei 28, 2023 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar, wenyeji Yanga kufungwa mabao 1-2.

Kwa misimu 5 mfululizo iliyopita mabingwa wa Afrika kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Africa wametoka ukanda wa kaskazini kanda ya (UNAF), timu ya mwisho kutwaa ubingwa wa michuano hii kutoka kanda tofauti ilikuwa TP Mazembe ya Congo mwaka 2017.
Ikiwa Juni 3, 2023 inatarajiwa kuchezwa mechi ya mkondo wa pili wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, wawakilishi wa Tanzania, Yanga SC wana kazi moja kubwa ya kuweka historia na kuvunja utawala uliowekwa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Kumbuka Yanga SC watakuwa uwanjani nchini Algeria kucheza dhidi ya USM Alger baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa Mei 28, 2023 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar, wenyeji Yanga kufungwa mabao 1-2.

Kwa misimu 5 mfululizo iliyopita mabingwa wa Afrika kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika wametoka Ukanda wa Kaskazini wanaowakilisha Kanda ya UNAF.

Timu ya mwisho kutwaa ubingwa wa michuano hii kutoka kanda tofauti ilikuwa TP Mazembe ya Congo ambayo inawakilisha Kanda ya UNIFFAC ambapo ilichukua mfululizo, mwaka 2016 na 2017.

Ili Yanga SC ifanikiwe kuwa bingwa, inapaswa kupata ushindi wenye uwiano wa mabao kuanzia 2-0 au ishinde 2-1 kisha penalti ziamue, la sivyo, stori yao itaishia hapo.

Endapo Yanga itafanikiwa kuwa bingwa wa michuano hiyo msimu huu, itakuwa timu ya kwanza kutoka Kanda ya CECAFA kubeba ubingwa huo kwani tangu mwaka 2004 ilipoanzishwa michuano hiyo, hakuna timu kutoka CECAFA iliyobeba ubingwa zaidi ya kushika nafasi ya pili ambayo ni Al Merrikh ya Sudan iliyocheza fainali mwaka 2007 dhidi ya CS Sfaxien, ikapoteza kwa jumla ya mabao 5-2 na kushika nafasi ya pili.

Hivyo hadi sasa Yanga wana rekodi yao ya kuwa timu ya pili kutoka CECAFA kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, wanaisaka rekodi mpya ya kuwa bingwa. Kila la kheri Yanga SC.

Katika miaka 19 iliyopita ya michuano hiyo, mabingwa wametoka kanda tatu pekee ambazo ni UNAF (Morocco, Misri na Tunisia), UNIFFAC (DR Congo na Congo) na WAFU (Mali na Ghana).

Kuhusu kanda, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limegawa Kanda Tano Kisoka kulingana na jiografia ya Bara la Afrika.

UNAF ni Kanda ya Kaskazini yenye wajumbe wafuatao; Algeria, Misri, Morocco, Libya na Tunisia.

WAFU ni Kanda ya Magharibi, hii imegawanyika A na B.

Wajumbe wa A ni Cape Verde, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau, Libya, Mali, Mauritania, Senegal na Sierra Leone.

Wajumbe wa B ni Benin, Burkina Faso, Ghana, Ivory Coast, Niger, Nigeria na Togo.
UNIFFAC (Central African Football Federations' Union) kuna nchi za Cameroon, Afrika ya Kati, Chad, Congo, DR Congo, Equatorial Guinea, Gabon na Sao Tome and Principe.

CECAFA ni Kanda ya Afrika Mshariki, wajumbe wake ni Tanzania, Kenya, Uganda, Zanzibar, Burundi, Rwanda, Djibouti, Ethiopia, Eritrea, Somalia, Sudan na Sudan Kusini.

COSAFA ni Kanda ya Kusini, wajumbe wake Afrika Kusini, Angola, Botswana, Comoros, Eswatini, Lesotho, Malawi, Mauritius, Madagascar, Msumbiji, Namibia, Seychelles, Zambia na Zimbabwe.

HII HAPA ORODHA YA MABINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA TANGU 2004:

2004 Hearts of Oak (Ghana)
2005 ASFAR (Morocco)
2006 Étoile du Sahel (Tunisia)
2007 CS Sfaxien (Tunisia)
2008 CS Sfaxien (Tunisia)
2009 Stade Malien (Mali)
2010 FUS de Rabat (Morocco)
2011 MAS Fez (Morocco)
2012 AC Léopards (Congo)
2013 CS Sfaxien (Tunisia)
2014 Al Ahly (Misri)
2015 Étoile du Sahel (Tunisia)
2016 TP Mazembe (DR Congo)
2017 TP Mazembe (DR Congo)
2018 Raja CA (Morocco)
2019 Zamalek SC (Misri)
2020 RS Berkane (Morocco)
2021 Raja CA (Morocco)
2022 RS Berkane (Morocco)
 
Utopolo hayana akili timamu, umekandwakandwa kwako, tena ukawa unaomba game ishe haraka, eti leo unajidai unaenda kupindua matako ugenini kwa mwarabu! Uto kuweni siriaz bas.
 
Mungu yule yule aliyeshusha mvua pale kwa Mkapa au Mungu yupi atakayewasaidia yanga?

Haya ni matumizi mabaya ya kuomba 😏
mungu hashushagi mvua za namna ile wewew mtoto mdgo hujui kitu kaa kimya...UCHAWI HAUVUKI BODA
 
Utopolo hayana akili timamu, umekandwakandwa kwako, tena ukawa unaomba game ishe haraka, eti leo unajidai unaenda kupindua matako ugenini kwa mwarabu! Uto kuweni siriaz bas.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mngekua mnatutakia na siso Simba kheri...leo tungekesha kwa mwamposya tukiwaombea ila kwa sbb na nyie mna midomo michafu na kuiombea mabaya Simba basi hilo kombe libaki ukanda huo huo...
 
Mngekua mnatutakia na siso Simba kheri...leo tungekesha kwa mwamposya tukiwaombea ila kwa sbb na nyie mna midomo michafu na kuiombea mabaya Simba basi hilo kombe libaki ukanda huo huo...
Tena itapendeza endapo wakakandwa hamsa bin dhofur ili wajue kbisa hawana timu.
 
6ce609b2-aa62-4cba-9f10-5a0cc1d4a109.jpg
 
Back
Top Bottom