Yanga SC kushuka daraja mwakani!

Yanga SC kushuka daraja mwakani!

Mkuu GENTAMYCINE Hiyo paragraph ya nne hiyo nimecheka balaa kwamba muda si mrefu bakora zitaanza kutembea mitaa ya Jangwani na Twiga. [HASHTAG]#thisissimba[/HASHTAG]

Yaani watachapana sana Mkuu kwani Simba SC na Azam FC ambao tuna ' Undugu ' tumeshaamua ' Kuibomoa ' na ' Kuimaliza ' kabisa Yanga SC. Itakuwa hivyo hadi watuombe msahama kwa madhila / mabaya yao waliyotufanyia wakati wa awamu ya Nne na ya yule ' Gabachori ' wao.
 
Mkuu,a one........siyo kiingereza ,umezingua au ndo Yale aliyoyasema mwana msimbazi mwenzio Rage?

Lugha Mama yangu ni Kinyarwanda, Kiganda, Kizanaki, Kimakuwa na Kiswahili na hicho Kiingereza chako / chenu wala sikipi sana Kipaumbele japo nakushukuru kwa Kunisahihisha ila sina uhakika pia kama Kujua Kwako Kiingereza kumekusaidia Kukuondolea umasikini / ukapuku wako uliokushamiri hadi katika Kope zako za macho.
 
Tshishimbi kamaliza mkataba Yanga?
Vp kuhusu Kichuya simuoni hapo.. au safari ya Tp mazembe imefika.

This is Simba

Ngoja niliweke hili wazi ili uwe ufafanuzi kwa wengine wote ambao wana swali au hofu kama yako. Ni kweli kwamba Tshishimbi aliingia Mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga SC ila katika ' Contract ' yake kuna ' Clause ' moja imeweka wazi kabisa kwamba endapo hatolipwa Mshahara wake ndani ya miezi mitatu mfululizo basi ' automatically ' mkataba wake utakuwa umevunjwa rasmi na siyo Siri kwamba Wachezaji wa Yanga SC wana zaidi ya hiyo miezi hawajalipwa mishahara yao kutokana na waya / ukame wa Pesa uliopo hapo. Wanachopewa sasa Wachezaji wa Yanga SC si mshahara ' as such ' bali ni ' allowances ' tu na ndiyo maana unaona hata Donald Ngoma aliwahenyesha Yanga SC huku akiwadanganya kuwa anaumwa wakati ukweli ni kwamba alikuwa haumwi bali aliona njaa imezidi na kuna malipo yake fulani fulani alizungushwa kulipwa na akaamua asuse na ' awatengeneze ' Yanga SC. Labda tu mambo yabadilike usiku huu ila Simba SC imeandaa ' mapigo ' mawili ' matakatifu ' Yanga SC ya kulipiza Kisasi cha Yondan na Twite ambapo iwe isiwe Tshishimbi na Chirwa wanaenda kutua Wekundu wa Msimbazi / Mnyama Mnyamani / Simba Sports Club.

Kichuya yupo bado Simba SC ila kama Le Tou Puisant Mazembe wataweka ' mzigo ' wa maana basi Simba SC itamuachia aende ili Pesa yake hiyo hiyo itusaidie katika Kusajilia ' majembe ' mengine kutoka Ghana au Nigeria au Zambia ambako ndiko kuna Wachezaji wa aina ya ' Kazi Kazi ' watakaotusaidia hasa katika michuano ya Kimataifa ya Klabu Bingwa Afrika.

Kila la kheri.
 
Quality Group Limited is Tanzania's largest conglomerate with 17 companies in the automotive, engineering products, international trade, logistic solutions and warehousing, real estate development, food processing, consulting, transport, aluminiumand fisheries sectors...Kawadanganye wanywa kahawa wenzako..kama ulikuwa hujui Manji ndio tajiri namba moja Tanzania... Quality Group ina thamani ya 13 Billion's... Tigo peke yake Manji anamiliki 99% ina thamani ya $ 1.4billion...Muulize Mo anavyomuogopa Yusuf.....alafu kuna jitu lingine lingine linaitwa Shubhash Patel hatari...wote wanarudi kundini 10 June....alafu Chirwa mchukueni hana hata footwork nzuri...Tshitshimbi hamuwezi kuvunja mkataba wake...
Kujifariji TIBA pia mkuu.
 
Day dreaming does not break any law.
Labda hela za Mo ni majini. Au wajanja wanapiga dili
Kwa bei ya billion 20, Simba could be the cheapest club in among the top four in Tanzania. Value ya Mbeya City ni 100 billions!
Siku si nyingi, Mo ataiuza Simba more than 50 billions.
Mark my words for your future reference.
Eti thamani ya mbeya city ni kubwa kuliko simba, upo serious mkuu?
 
Sibishani na Watu waliojifunza mpira juzi, jana na leo tafadhali. Nenda Kwanza kajifunze mambo ya mpira hasa huu wa Bongo na ukiona umeshafuzu rudi Kwangu tafadhali. Halafu siku nyingine uwe unajitahidi sana kuuficha Upopoma / Upumbavu wako kwani unajidhalilisha leo hii ukimfananisha ' Tajiri ' Kijana Afrika na ' Tajiri ' namba moja Tanzania Mohamed ' Mo ' Dewji na ' Msanii ' wa mjini Yusuph Manji. Kuna Watu huwa ' mnakera ' hadi tunakosa uvumilivu juu yenu. Yaani sijaishia tu kukupuuza bali pia nimekudharau sana na sishangai Wana Yanga SC wengi uwezo wenu wa Kufikiri na Kujenga hoja ni haba kama siyo finyu sana na haishangazi mpaka leo bado Klabu yenu ' inaogelea ' tu pale katika ' hazard area ' Jangwani na mnazungukwa tu na ' mafuriko ' kila uchao.
 
Hivi una ' akili ' timamu kabisa kweli Wewe?
 
ukiona MTU anatukana hana facts..
Yusuf Manji, the CEO of Quality Group Tanzania and one of the richest men in Africa, was born into a life of privilege. Highly intelligent and educated in the US he took over his family business and grew it into one of the most successful businesses in Tanzania

As a highly intelligent man, Yusuf Manji has been unable to refrain from going overboard, taking his family with him..Manji hawezi kuwekwa Forbes maana ni family business wewe kilaza...niambie kampuni moja ya Mo yenye thamani ya Tigo...... Ingia YouTube Mkasi ya Salama mwenyewe Mo alisema alienda kukopa bank South Africa $250m..billionaire anakopa????Mzee Dalali alilia Simba kuchukuliwa kwa 20B akatoa mfano wa Manji kuivalue Yanga 40 B..
 
Ukishawasajili wachezaji wote wa Yanga huidhofishi Yanga bali unaipa ahueni ya kujenga timu nzuri zaidi.
Halafu Yanga ni taasisi kubwa sana kila mwenye uwezo angetamani kuwa sehemu yake. Ni swala la muda tu Yanga itasimama tena na msimu ujao jiandaeni kuiona Yanga bora zaid.
Kilichokwamisha Yanga ni watu wanaoitwa wazee, Manji alikuwa na mpango mzuri kuliko hata kiasi alichowekeza MO lakini kwa ujinga wa baadhi ya wanachama wakavuruga mchakato ule kwa maslahi yao binafsi, tujiulize wale walioenda mpaka mahakamani wako wapi kipindi hiki timu haina muelekeo?
Nilichowasifu Simba ni kuwapuuza wanaoitwa wazee na wasaliti wachache, mchakato umeenda na kuwaacha wasaliti wakiwa hawana cha kusema mbona matunda yameonekana.
Subiria kwenye mkutano mkuu wa Yanga Akili mali na wenzake watie pua pale ndio utaona hasira za wananchi, mpaka sasa hivi ajenda kubwa ya wanachama ni Mzee Akili mali na wenzake, atakachopata hatasahau maishani mwake na kwa karne hii mpira hauwezi kuchezwa kama burudani tu bali biashara zaidi. Kingine Yanga ilikosa viongozi wenye macho ya kuongoza mpira, huwezi kubwa na viongozi katika karne hii wanaowaza uzalendo kwenye mpira, yaani wachezaji wacheze tu bila mishahara kwa kisingizio cha uzalendo, yaani Chirwa, Ngoma na wengine wawe wazalendo kwa Yanga! Hata timu ya taifa hatufanyi hivyo.
Mwisho kabisa, Yanga inahitaji viongozi wapya wenye uwezo wa kuongoza mpira na sio vikundi vya uzalendo.
 
Eti thamani ya mbeya city ni kubwa kuliko simba, upo serious mkuu?
Hivi unaamini Simba ina value ya 20 billions za Mo?
Yes Mbeya City itakuwa kampuni kwa value hiyo ya 100 billions. Hapo utajua nini kinaendelea Simba. Wenye akili ndani ya Simba wameliona hilo na kuanza kupiga kelele. Wanaitwa wasaliti.
Hapo juzi Kati nusura Haji ajitoe Simba. Njaa mbaya sana. Kawekwa sawa dakika sifuri aendelee kuimba kama kasuku.
Tusubiri Simba ya Mo ndani ya mwaka mmoja tu.
 
Mikia endeleeni kujipa moyo,Yanga inayotengenezwa ndani na nje ya uwanja huyo mo wenu km hajakimbia km alivyozikimbia singida utd na lyon sijui
 
Yaani watachapana sana Mkuu kwani Simba SC na Azam FC ambao tuna ' Undugu ' tumeshaamua ' Kuibomoa ' na ' Kuimaliza ' kabisa Yanga SC. Itakuwa hivyo hadi watuombe msahama kwa madhila / mabaya yao waliyotufanyia wakati wa awamu ya Nne na ya yule ' Gabachori ' wao.
Acha Kupotosha AZAM FC Hatuna Undugu na MIKIA.... pamabneni na hali zenu..
 
Baada ya Azam FC kumalizana na Donald Ngoma na muda si mrefu wanaenda kumalizana na akina Thabani Kamusoko na Kelvin Yondani taarifa zilizonifikia hivi punde zinasema kwamba muda wowote Kiungo Papy Tshishimbi na Mshambuliaji Obren Chirwa wanasaini kuichezea Simba SC.

Je Yanga SC itakuwepo mwakani?

Poleni sana Yanga. Mlianza sasa tunamaliza kudadeki.

Mpaka mje mtuombe radhi Simba SC ndipo tunaweza kufikiria kuwasamehe ila nina uhakika kwa kuondoka kwa Ngoma, Kamusoko, Yondani, Tshishimbi na Chirwa tayari Yanga SC imeshashuka daraja rasmi katika Ligi Kuu ya msimu ujao wa 2018 / 2019.

Kama ambavyo mlitutesa Simba SC kwa akina Kelvin Yondan na Mbuyi Twite kupitia ' Tajiri ' wenu Yusuph Manji sasa nasi Simba SC kupitia si tu Tajiri bali ni ' Bilionea ' Mohamed Dewji sasa tumeamua kulipiza Kisasi na najua kuwa kwa taarifa hii ya Tshishimbi na Chirwa kusaini Simba SC muda wowote kuanzia sasa litakuwa ni ' Pigo ' moja takatifu kwa Yanga SC huku niamini kuwa muda wowote ule ' Bakora ' zitaanza kutembea pande za mitaa ya Twiga na Jangwani.

Wana Simba SC popote pale mlipo kaeni tayari kuwapokea hawa Wachezaji wawili akina Tshishimbi na Chirwa kwani tayari ' almost done deal ' na mliokuwa leo maeneo ya Posta karibu na Ofisi ya ' Bilionea ' kuna mambo mliyaona. Simba SC sasa hivi hatutanii na tunatumia Pesa kwa raha zetu na mtatutambua mwakani.

Simba SC 2018 / 2019
  1. Aishi Manula
  2. Shomari Kapombe ' Kiraka '
  3. Asante Kwasi
  4. Paul Bukaba
  5. Erasto Nyoni
  6. Jonas Mkude
  7. Haruna Fadhil Hakizimana Niyonzima ' Niyo Fabregas '
  8. Papy Kabamba Tshishimbi
  9. Obren Chirwa
  10. John Raphael Boko ' Adebayor '
  11. Emanuel Okwi
Kwa Kikosi chetu hiki Kipya cha Msimu ujao niwaombe tu TFF watukabidhi mapema Kombe letu kwani kuna uwezekano mkubwa sana Simba SC tukachukua ' Ubingwa ' zikiwa zimebaki mechi 15 huku idadi ya magoli yetu ya Kufunga yakiwa 203 na ya kufungwa yakiwa ni 0.

Nawasilisha.
Na kale kamlungula ka Mo....maana mechi halali ni ile moja mbele ya mkuu pale kwa mchina dhidi ya Kagera Sukari.
 
Back
Top Bottom