Yanga SC mabeki wakiwa Moro na Ninja tunakula 7, ila wakiwa Nondo na Job tunakula 5 hivyo tuchagueni mapema 'Kifurushi' chetu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Ushauri wangu wa bure tu Kwenu Watani zangu Yanga SC kama itawapendeza ili angalau Kupunguza idadi ya Magoli ya Kufungwa na Simba SC Jumamosi tarehe 8 May, 2021 yawe 3 kwa 0 (ambayo ndiyo nayaona Kiutabiri) kuwa mtafungwa Mchezaji Tonombe Mukoko namba 5 na Juma Makapu namba 4.

Mkiwapanga Moro na Ninja naziona Penati Nne (4) na Kadi Nyekundu Mbili Kwao kwa Uchezaji wao wa 'Kibangebange' uliozoeleka.

Mkiwapanga Nondo na Job naziona Penati Mbili (2) na Kadi Nyekundu Moja kwa Uchezaji wao wa 'Kimataputapu' uliozoeleka hasa kwa Nondo 'akishalewa' hivyo.

Bado Siku zipo hivyo nawashauri Yanga SC ama 'gomeni' Kucheza Mechi hiyo au anzeni mapema tu kutafuta 'Visingizio' vya kuwapa Mashabiki wenu ambao najua kwa Kipigo cha 'Kishalubela' mtakachokipata Siku hiyo watafanya Fujo kubwa kwa Viongozi na hata kwa Wachezaji wa Yanga SC.

Halafu acheni 'Kulazimisha' Winga wenu Tuisila Kisinda acheze hiyo Mechi huku kuanzia leo huko Mazoezini Kwenu kuanza 'Kumdunga' Sindano za Ganzi ili aanze Kuzizoea. Mnamtesa bure 'Bandeko Nangai' Mkongo wa Watu na Jeraha lake halitapona haraka.

Yaani nawaoneeni mno Huruma Yanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…