Yanga SC yaiangukia serikali

Yanga SC yaiangukia serikali

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Kikosi cha Yanga kimeamua kujisalimisha kwa serikali kwa kuandika barua ya kuomba radhi ili waweze kuruhusiwa kuweza kutumia Uwanja wa Taifa baada ya kuzuiliwa kwa muda usiojulikana.

Hatua hiyo ya kuiandikia barua serikali imekuja baada ya ombil lao la kutumia Uwanja wa Amaan, Zanzibar kugoga mwamba.

Hatua hiyo ya yanga imekuja baada ya siku chache Simba nayo kuandika barua kuomba kuruhusiwa kutumia Uwanja wa Taifa, ambapo wiki iliyopita serikali kupitia kwa waziri wenye dhamana ya michezo Nape Nnauye ilizipiga marufuku Simba na Yanga kutumia uwanja huo kutokana na uharibifu wa viti na meza uwanjani hapo.

Pia serikali ilizitaka timu hizo kuweza kuwajibika na uhalibifu wa mali hizo, huku ikiendelea na kifungo.

Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania, Alfred Lucas amesema, Kikosi cha Yanga waliandika barua ya kuomba radhi ambapo majibu yake yanatarajiwa kutolewa leo au kesho kwani wanamchezo zidi ya Mtibwa.

Lucas amesema, mpaka jana TFF walikuwa hawajajua mchezo huo utachezwa katika uwanja gani kwani mchezo huo unatarajiwa kuchezwa siku ya Alhamisi, kwani Uwanja wa Uhuru bado unahitaji matengenezo zaidi.

“Kama walivyofanya Simba na Yanga nayo imeamua kuandika barua ya kuomba radhi ili kuweza kusamehewa na kuendelea kuutumia uwanaj huo na majibu hayo yanatarajiwa leo au kesho ili kujua itakuwaje,” amesema Lucas.

Kwa upande wa matajiri Azam, kupitia makamu mwenyekiti wao, Idrisa Nassor amesema, wapo tayari kuipokea timu yoyote itakayoomba kuutumia uwanja wao wa Azam Complex uliopo Chamazi, Mbagala jijini Dr es Salaam, kama serikali ikiendelea kuwawekea ngumu.

“Timu yoyote kati ya hizi ikiamua kuja kuomba kuutumia uwanja wetu tutawapa kwani hatuna ugomvi na timu yoyote kati ya hizo,” amesema Nassor.

Chanzo: Hivi Sasa
 
Back
Top Bottom