Yanga SC Yapanda Namba 9 Viwango Vya Klabu Bora Afrika

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Hii ni orodha ya matokeo ya viwango vipya ambavyo vimetolewa na Shirikisho laa Kimataifa la Takwimu na Historia za Mpira wa Miguu yaani (IFFHS)

Link:- (IFFHS)

Kongole kwa GSM kwa maana jitihada zako zisizo na mbambamba zimefanya Mabingwa wa kihistoria wa LigiKUU Tanzania Kushika nafasi ya 9 ambayo haijawahi kufikiwa na Klabu yeyote ile kutoka ukanda wa nchi waasisi za Afrika Mashariki.

Natumai baada ya kuchukua ubingwa wa CAFCC tutafika hadi nafasi ya 2 kiafrika.

Matunda ya uwekezaji bora, usajili bora na uendeshaji bora wa kisasa wa klabu ndio haya sasa.
 
Chadema watapinga
Siyo chadema watakaopinga ila wale wanaotaka Yanga "ife kiume" pia. Hata kama data walizotumia jamaa hao siyo za kuaminika, kiwango cha yanga kiko juu sana kwa sasa hivi. Best ten wao wana timu chache sana zilizobaki kwenye mashindano ya CAF nadhani nne au tano hivi wakati timu nyingine zilizobaki ni wale waliokwishatolewa kwenye mashindano ya CAF au ambao hawakushiriki kabisa katika mashindanno ya CAF mwaka huu.
 
Shukrani mkuu
 
Hakuna kitu kinaitwa masindano ya CAF.
Kuna CAF champions league na CAF Confederation Cup.
Moja ni ligi nyingine ni kikombe.
Kama Ilivyo UEFA na EUROPA.
Najua unayafahamu haya, ila nakazia tu.
 
Hakuna kitu kinaitwa masindano ya CAF.
Kuna CAF champions league na CAF Confederation Cup.
Moja ni ligi nyingine ni kikombe.
Kama Ilivyo UEFA na EUROPA.
Najua unayafahamu haya, ila nakazia tu.
Umeona wapi LIGI ina makundi [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Simba watakataa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…