Yanga, Simba na Azam zapata shavu Russia

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Klabu za Simba, Yanga na Azam zimepata fursa ya kucheza mechi za kirafiki na klabu za Ligi Kuu ya Russia, pamoja na kuweka kambi katika kipindi cha mapumziko ya ligi.

Fursa hiyo imepatikana kutokana na ziara ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro nchini humo na alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Michezo wa nchi hiyo, Mikhail Degtyarev, Desemba 3, 2024.
 
Labda mimi ndo sijaelewa, hivi kwenda huko kunahitaji ruhusa au maamuzi na uwezo wa kifedha wa timu ?
 
Waziri simkubali ase, mkoani kwake hamna hata team ligi kuu
 
MOSCOW, Urusi: KLABU za Simba, Yanga na Azam za Ligi kuu ya Tanzania Bara zimepata fursa ya kucheza mechi za kirafiki na Klabu za Ligi kuu ya Urusi pamoja na kuweka kambi kwa timu hizo katika kipindi cha mapumziko ya ligi kuu.

Fursa hiyo imepatikana kufuatia ziara ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Damas Ndumbaro nchini humo ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Michezo wa nchi hiyo, Mikhail Degtyarev.

Pamoja na fursa hiyo Waziri Ndumbaro amependekeza kuwapo na ushirikiano wa kubadilishana utaalamu katika ngazi ya vilabu pamoja na kuwa na michezo ya mara kwa mara ya kirafiki baina ya vilabu vya ligi mbalimbali za nchi hizo mbili.

Aidha, Waziri Ndumbaro ametembelea ofisi za Bodi ya Ligi Kuu ya Urusi na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Muendeshaji Mkuu wa bodi hiyo, Evgeniy Melezhikov ambapo wamekubaliana kuanzisha ushirikiano baina ya timu za taifa na kuwa na mechi za kirafiki.

20241205_140530.jpg

#HabarileoUPDATES
 
Ningesikia zinaenda kucheza na Chelsea, Liverpool au Man City kidogo ningeona ni fursa
 
MOSCOW, Urusi: KLABU za Simba, Yanga na Azam za Ligi kuu ya Tanzania Bara zimepata fursa ya kucheza mechi za kirafiki na Klabu za Ligi kuu ya Urusi pamoja na kuweka kambi kwa timu hizo katika kipindi cha mapumziko ya ligi kuu.

Fursa hiyo imepatikana kufuatia ziara ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Damas Ndumbaro nchini humo ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Michezo wa nchi hiyo, Mikhail Degtyarev.

Pamoja na fursa hiyo Waziri Ndumbaro amependekeza kuwapo na ushirikiano wa kubadilishana utaalamu katika ngazi ya vilabu pamoja na kuwa na michezo ya mara kwa mara ya kirafiki baina ya vilabu vya ligi mbalimbali za nchi hizo mbili.

Aidha, Waziri Ndumbaro ametembelea ofisi za Bodi ya Ligi Kuu ya Urusi na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Muendeshaji Mkuu wa bodi hiyo, Evgeniy Melezhikov ambapo wamekubaliana kuanzisha ushirikiano baina ya timu za taifa na kuwa na mechi za kirafiki.

View attachment 3169509

#HabarileoUPDATES
Na wako banned na FIFA & UEFA hawana faida yoyote
 
Back
Top Bottom