YANGA: Taarifa kwa Watanzania

YANGA: Taarifa kwa Watanzania

Hii UTOPOLO sasa imekuwa ze Comedy yani wanafukuza wajumbe kwa kuwa Gharib imesitisha Kufanya mambo yasiyomuhusu?

Yeye kazi yake ni kutengeza vijora vya Vyura fc 🐸 🐸 acheni shobo.
kwa kweli hili linashangaza sana. uongozi unapogeuka kuwa wapambe na kumlamba matako sponsor
 
kwa kweli hili linashangaza sana. uongozi unapogeuka kuwa wapambe na kumlamba matako sponsor
Jamaa kaamua heri ale ugali kwanza
20200329_205645.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mlimganda Manje awe anawapa pesa za bure kama vile anampa mkewe akakupotezeeni

Sasa tena mmeanza kumganda GSM awe anawapa pesa za bure jamani hayo mambo yameshapitwa na wakati badirikeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Yanga SC umewasimamisha wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji, Salim Rupia na Frank Kamugisha kuanzia leo Machi 27, 2020 hadi hapo mkutano mkuu utakapofanya maamuzi kwa mujibu wa katiba.

Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa klabu, Dkt. Mbette Mshindo Msolla leo, imesema kwamba uamuzi huo umefikiwa leo baada ya kikao cha siku mbili mfululizo kilichofanyika Dar es Salaam kuanzia Mach 26 hadi 27.

Na hatua hiyo imefuatia kutokea sintofahamu iliyosababisha mdhamini wa klabu, Kampuni ya GSM kusitisha kutoa misaada iliyo nje ya mkataba wake.

Aidha, Kamati ya Utendaji ya Yanga imepokea na kukubali maombi ya wajumbe wengine watatu, Rodgers Gumbo, Shijja Richard na Said Kambi kujiuzulu nafasi zao na kwamba nafasi ya mjumbe wa kuchaguliwa itajazwa mara moja kwa mujibu wa Ibara ya 29(3) wa Katiba ya Yanga.

Wakati huo huo Kamati ya Utendaji wa Yanga imewasilisha barua GSM kujibu barua yao yenye kumbu kumbu namba GSMGROUP/YANGA/LETTER/2/2020 ya tarehe 24/03/2020 kuhusu kujitoa udhamini wa maswala yasiyo ya kimkataba.
Taarifa ya Mwenyekiti, Dk. Msolla imesema kwamba Barua hiyo imewasilishwa baada ya maamuzi ya pamoja ya kikao cha Kamati ya Utendaji leo.

Shijja na Kambi walikuwa Wajumbe wa kuteuliwa wakati Rupia, Kamugisha na Gumbo ni miongoni mwa Wajumbe waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Mei 5, mwaka jana Jijin Dar es Salaam.

Sasa Kamati ya Utendaji Yanga inabaki na Wajumbe watano wa kuchaguliwa ambao ni Hamad Islam, Mhandisi Bahati Faison Mwaseba, Dominick Ikute, Arafat Haji na Saad Khimji pamoja na Dk. Athumani Kihamia pekee wa kuteulwa chini ya Mwenyekiti Dk. Msolla na Makamu Mwenyekiti, Frederick Mwakalebela.
Gr8D01p9--M

Wakati huo huo Kamati ya Utendaji wa Yanga imewasilisha barua GSM kujibu barua yao yenye kumbu kumbu namba GSMGROUP/YANGA/LETTER/2/2020 ya tarehe 24/03/2020 kuhusu kujitoa udhamini wa maswala yasiyo ya kimkataba.
Taarifa ya Mwenyekiti, Dk. Msolla imesema kwamba Barua hiyo imewasilishwa baada ya maamuzi ya pamoja ya kikao cha Kamati ya Utendaji leo.

Hamuoni hata aibu kama GSM ameamua kusitisha kukupeni pesa za bure ambazo hazipo katka mkataba sasa mnalialia nini hadi mnamuandikia na barua kwani kutoa msada ni lazima?

Kitu ambacho mnatakiwa mfanye ni kuifanya Yanga ijitegemee sio kutaka mpewe pesa za bure kila siku

Kama kazi imewashinda tokeni waingie watu wanaojua wasio penda kuombaomba ili waifanye Yanga iwe ni clabu inayojitegemea

Brand ya Yanga inawezo wa kuingizia Yanga pesa na ikaendesha mambo yake bili ya kulialia kutaka mpewe pesa za bure

Nendeni mkawafufue akina Gulamali waendelee kukupeni pesa za bure sijui walikuwa wanazipata wapi na sijui zilikuwa zinarudi vipi kwao

Nyinyi viongozi wa Yanga sasa kila siku mnazidi kututia aibu

GSM usitoe hata shilingi moja ambayo haipo katika mkataba wako hiyo ndio dawa ya mambumbu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom