Yanga tuache kulalamika

CAGvsSPEAKER

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2019
Posts
1,339
Reaction score
5,048
Mimi ni mwanaYanga tena Yanga kweli.

Yanga bado ni mbovu. Tukubali hilo kwanza. Pia, viongozi na muhamasishaji wetu wasiwajengee mashabiki hisia za kuonewa.
Kweli Yanga ingekuwa imara ilikuwa ya kutoa suluhu na Gwambina? Na tukubali tu kuwa muelekeo ulianza kupotea pale.

Tuliitukuza mechi na mtani tukaacha kujihakikishia pointi tatu kutoka kwa Gwambina, matokeo yake mechi mbili tukaambukia pointi 2 kitu ambacho tungeshinda ya Gwambina na kutoa sare na mtani zingekuwa ni point 4.

Jana tumesare na Mbeya City, analaumiwa refa yale mashuti alokuwa anapiga Sarpong huko mawingini tulitaka refa aite mpira kati?
Timu bado ni mbovu nashangaa mashabiki wanaingia kwenye mtego wa viongozi wa kuwalaumu marefa uyo Saido ni pancha tupu, Kalinyos ndo usiseme, Yakuba pancha na kocha anatumia kilichopo siwezi kumlaumu.

Tukubaliane kuwa,timu yetu bado ni mbovu. Jana walicheza hovyo kuliko hovyo nyingine zote. Mbeya City waliwalazimisha kucheza walivyotaka. Ilikuwa puu paaa utadhani huo mpira una moto.

Badala ya viongozi kuwaambia mashabiki ukweli, wao wanawaaminisha kuwa refa ndo tatizo. Hizi timu mnazozidharau zilikuwa busy kujiandaa na raundi yapi......sisi tulikuwa busy kwenye vyombo vya habari kusaji na media sijui nini.

Nihitimishe, WanaYANGA,mtani hayupo mbali na sisi ubingwa tunaweza kuendelea kuusikia tena kama viongozi hawatakuwa serious.

Pia ni wakati sasa wa Fredrick Lugano Mwakalebela kujitafakari kama anaendelea kutosha katika kiti anachokalia sasa. Tarehe 12 Feb imepita hatujasikia yeye au kiongozi yoyote wa Yanga alokwea ndege kwenda CAS kusikiliza kesi ya Yanga na Morison.
Wala si Morison au kiongozi yoyote wa Simba aliyekwenda CAS kwa shauri hilo.

Niendelee kuimbea Yanga yetu ule muujiza wa kutaka Ubingwa na ubovu tulionao utimie msimu huu walau na sisi tufurahi kidogo.
Tukutane tarehe 17 na Kagera ambao nao sidhani kama watakuja kushangaa Mfugale au Ubungo interchange.

Mungu awe nasi.

Yanga, DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO.
 
Siku Yanga wakija kugundua kocha ni mbovu mda utakuwa umeenda sana mana jana haijulikani timu ilikuwa inacheza mfumo gani
Kocha wa Yanga siyo mbovu ila ni mbinafsi. Mapenzi kwa Sarpong hayana sababu za msingi. Kosa la refa ni moja tu mechi nzima ya Jana, kujifanya hajaona Kaseke alipofanyiwa faulo ndani ya 18 kabla ya krosi kumfikia.
 
Mkuu umenena vizuri sana, ila hiyo kauli yenu ya DAIMA MBELE NYUMA MWIKO inaukakasi kidogo huo Mwiko kwanini mmeweka nyuma au hamuwezi kuuchomoa??
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]we jamaa wewe!!
Nimecheka sana.
 
Siku Yanga wakija kugundua kocha ni mbovu mda utakuwa umeenda sana mana jana haijulikani timu ilikuwa inacheza mfumo gani
Bado sijamlaumu kocha wachezaji wengi wanatakiwa kuwa Mwadui au Ihefu pale ukianza kujenga timu utaanza na Metacha, Shikalo, Mukoko, Tuisila(japo naye kuna mida mikimbio yake haina maana), Feisal, Kaseke, Yasin, Kibwana, Lamine na Mwamnyeto wengine wote fukuzia mbali.
 
Uwanja wenyewe nao ulikuwa kama majaruba ya kupandia mpunga!! Fiston bado hana game fitness lakini mwalimu alimuacha tu apuyange uwanjani kwa dakika zaidi ya 70!

Faridi Mussa na Sarpong walitakiwa kupumzishwa mapema! All in all, ukosefu wa umakini kwa mabeki kwa zile dakika za majeruhi, ulitukosesha point 3 muhimu baada ya kusababisha ile penati ya kizembe.

Lakini siyo vibaya pia kuwapongeza Mbeya City. Wamefanya usajili mzuri. Yule Mrundi wao mwenye jina la Didier nani sijui, kwa mechi ya jana alikua ni bora zaidi kuliko Mrundi mwenzake Fiston, lakini pia mshambuliaji wetu 'butu' Sarpong.
 
Mpira wa Tanzania una Mambo mengi nje ya uwanja, Haieezekani rafu aliyo chezewa Kaseke ndani ya eneo la Hatari maamuzi asione wakati Yuko mita 15 kutoka ilipo fanyika rafu na mshika kibendera asione pia na Yanga unawataka wasiseme lililo wanyima nafasi ya kushinda uo itakua wehu. Yaani atarefa ikitokea kapewa adhabu Yanga hainufaiki kwa lolote na Bado unashauri Yanga wasi kemeee!!!
 
Hivi hilo kosa akifanyiwa yanga ndio faulo akifanyiwa Luis anakuwa kajiangusha!

Ni mara nyingi sana Luis anaangushwa ndani ya box na hata yanga wenyewe wamemchezea mieleka ndani ya box na mwamuzi akapotezea
Kocha wa Yanga siyo mbovu ila ni mbinafsi. Mapenzi kwa Sarpong hayana sababu za msingi. Kosa la refa ni moja tu mechi nzima ya Jana, kujifanya hajaona Kaseke alipofanyiwa faulo ndani ya 18 kabla ya krosi kumfikia.
 
Faulo aliyo fanyiwa Kaseke ni shambulio la makusudi kwakua alikua anawania kwenda kufunga kabla mpira haujamfikia akarukiwa mgongoni na akashindwa ku ucheza mpira aliotakiwa afunge goli na wala haihusiani na kujiangusha kwa Namna yoyote ile.
 
Mkuu umenena vizuri sana, ila hiyo kauli yenu ya DAIMA MBELE NYUMA MWIKO inaukakasi kidogo huo Mwiko kwanini mmeweka nyuma au hamuwezi kuuchomoa?
Daima mbele nyuma mwiko

We jamaa mkorofi sanaa

Huo mwiko una shaka?
Una shaka?

[emoji38][emoji38]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…