Yanga tuache pressure, turudi tujenge timu

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2020
Posts
2,946
Reaction score
2,932
Kutokana wacheji wapya kutokuwa pamoja na kuzoeana,matokeo haya yasitutishe wala kutukatisha tamaa,tunawachezaji wazuri wakikaa pamoja kwa muda mrefu tutakuwa na timu bora kabisa.

Wale wenzetu wa porini wamekula biliani lenye nzi. Wametest mitambo butu, wasubiri vichapo tu mwaka huu

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Dar es salaam young African, tuna timu nzuri ila tutulie tujenge timu na tuache kusajili Kila msimu

Tuwaachie wachezaji wetu waungane vizuri tuchukue kombe la ligi kuu Ili mwakani twende kimataifa bila mbeleko
 
Hiki kikosi sikutegemea kufanya vzr kimataifa hata kidogo kwa hiki kikosi tukiache hadi msimu ujao hakuna kusajili sana pale ni kujazia nafasi mbili tulizonazo za kimataifa na labda kuuacha saidoo ambaye kwake umri ni tatizo
 
Muhimu tusisikie mchezaji kuuzwa, au kusitishiwa mkataba bila sababu za msingi. Mwalimu aendelee kuijenga timu.

Naamini tuna uwezo wa kuchukua ubingwa wa ligi kuu msimu huu, halafu mwakani tunarudi tena Kimataifa.
 
Kwanza kabisa Msola na Eng. Hersi wakae pembeni timu iongozwe na watu wenye maono ya mbali. Tutafanikiwa ila kama ndio hawa hawa viongozi basi tutaendelea kuwa wakusindikiza
 
Mwaka wa nne huu bado mnajenga timu au mnatangaza biashara
Kujenga timu si kitu cha mchezo na tena ukiangalia huko nyuma ukata uliopitiliza,ukiangalia kiundani mwaka wa pili huu ndio Yanga wanatengeneza timu serious baada ya gsm kuweka pesa ya maana,huko nyuma ilikua tunasajili wachezaji wa kuunga unga
 
Dar es salaam young African, tuna timu nzuri ila tutulie tujenge timu na tuache kusajili Kila msimu

Tuwaachie wachezaji wetu waungane vizuri tuchukue kombe la ligi kuu Ili mwakani twende kimataifa bila mbeleko
Nilijua mechi ya leo itawaonesha ubovu ubovu uko wapi, lakini bado mnajipa moyo eti timu nzuri.

Nashindwa kuelea sijui kwasababu mechi imechezeka kizani hivyo hamjapata wasaa wa kuona ubovu au ni kwasababu simba nayo imefungwa hivyo kuchukulia kirahisi matokeo mliyo pata?
 
Muhimu tusisikie mchezaji kuuzwa, au kusitishiwa mkataba bila sababu za msingi. Mwalimu aendelee kuijenga timu.

Naamini tuna uwezo wa kuchukua ubingwa wa ligi kuu msimu huu, halafu mwakani tunarudi tena Kimataifa.
Kurudi tena kimataifa ni mpaka Simba tuamue,tusipoamua amrudi.
Ombeni msamaha tuwabebe tena mwakani.
 
Bado hawana chemistry mzungu pori bhana
 
Kila mtu ana mtizamo wake, usitake tufanane
 
Tuacheni masihala ndugu zangu wanajangwani hatuna timu ya kucheka michuano ya nje labda kwenye ligi yetu humu ndani na bado tunapambania nafasi ya pili na ya tatu tu.

Huwa naumia sana kujipa moyo wakati tunauona kabisa ukweli. Hii timu haiwezi kuleta changamoto kimataifa hata mbele ya Simba tu mi nawaambia ukweli.

Tutaendelea kuwa watu wa kulia lia tu mara sijui Tff mara marefa mara sijui wananunua mechi n.k ila vyote hivyo visingizio tu. Hatuna kikosi cha uhakika kushindana ukizingatia kabisa tulijua tunaingia kombe la CAF tena tunaazia hatua za awali kabisa ambazo ni ngumu kweli kweli lakini watu hawako serious na kazi wanaleta uswahili swahili tu. Badala tuwekeze kusajili wachezaji wa maana mnaleta masihara hao wazee mnategemea kutengeneza kikosi nao? Acheni masihara mie nimekataa kujifariji kiboya namna hiyo tumechoka tunataka timu yenye kurudisha heshima ya Yanga na sio huu usanii.

Viongozi wa Yanga niwakumbushe tu kitu, Yanga sio chama cha siasa hiyo ni klabu ya michezo hasa mpira wa miguu ambao unatakiwa kupata matokeo mazuri na ubingwa yaani kifupi tunataka vikombe jangwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…