Yanga tusiache ile imani yetu ya jezi nyeusi

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Yanga turudie imani ile ya jezi nyeusi jezi ya kiama jezi ya moto. Najua wengi watanitukana na kuniambia kuwa jezi nyeusi haichezi mpira. Ila jezi nyeusi ni imani ambayo wana Yanga wamejiwekea.

Kama simba walivyo weka imani kuwa kwa mkapa hatoki mtu sio kwamba hatoki mtu wanatoka tena vizuri ila imani yao ambayo wamejiwekea ni kubwa kuliko hata team wanayo cheza nayo hata ikiwa kubwa kiasi gani kwasababu wana amini kuwa kwa mkapa hatoki mtu ndugu yangu kutoboa hapo ni kazi sio uchawi ila ni imani tu. Mtu ukiwa na imani ya kitu fulani hata kama hukiona ila utahisi uwepo wa kitu hicho.

Hata wachezaji wa Yanga wenyewe wameshawahi kusema kuwa wakivaa jezi nyeusi huwa wanahisi nguvu fulani mwilini. Ile nguvu ndo imani na sio kwamba ni uchawi ila hiyo ni kazi ya saikolojia mchezaji anahisi ana nguvu kubwa kumbe wapi. Kwa hiyo mazembe tukimvalia jezi nyeusi hatoboi.
 
Hii niliongelea kabla hata ya mechi ya Monastir. Matokeo ya mchezo wa mpira unabebwa na mambo mengi ukiachana na mbinu na ufundi. Kuna bahati na spirit ya upmbanaji. Jezi nyeusi ya Yanga imebeba sana timu katika matokeo lakini kwa kukosa maono zinazinduliwa jezi mpya pasipo kufikiria rangi iliyoibeba timu kwa bahati.
 
Mazembe mwenyewe ana jezi nyeusi
Kwenye kundi zinazovaa jezi nyeusi hazifiki mbili na hawawezi kufikiria kuvaa jezi nyeusi kwa michezo yote dhidi ya Yanga kwasababu kuna mahali mwenyeji ndio anayeamua jezi ya kuvaa.
 
Inafikirisha kuona tp mazembe wapo Caf confederation cup halafu horoya ipo Caf champions league kwa mkapa kuna aibu inakuja .

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…