Yanga tusiwabeze kabisa Club Africanais

Yanga tusiwabeze kabisa Club Africanais

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Baada ya draw ya leo mchana play off Kombe la Shirikisho, nimesikia maoni mengi ya wenzangu wakiitaja timu pinzani yetu kuwa ni wepesi na kwamba tutawapiga kama ngoma. Naomba tusijiamini hivyo wala kujipa imani kubwa itakayotutoa ari ya upambanaji.

Nijuavyo mimi Club Africanais ni wazuri hasa, kumfunga Kipanga goli 7 si kubahatisha, walimfunga kweli. Na Kipanga kutoa sare kule Zanzibar, si kwamba Kipanga alishindikana kufungwa bali wale Waarabu walichukua muda mwingi kuwasoma Kipanga kwa ile 1st leg.

Hivyo tusibweteke kabisa na kuchukulia wale walitoa draw na Kipanga, ati sisi itakua kazi rahisi tusijidanganye! Cha kufanya tukaze buti tupambane na kushinda idadi itakayowezekana ya magoli kwa mechi hiyo mkondo wa kwanza kabla ya kurudiana tarehe 9. Hiyo ndiyo silaha pekee tuliyonayo na si kuwabeza Waarabu.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Hamjakoma kudharau wenzenu
Kweli ninyi ni sikio la kufa
 
Baada ya draw ya leo mchana play off kombe la shirikisho
Nimesikia maoni mengi ya wenzangu wakiitaja timu pinzani yetu kuwa ni wepesi na kwamba tutawapiga kama ngoma,naomba tusijiamini hivyo wala kujipa imani kubwa itakayotutoa hari ya upambanaji

Nijuavyo mimi Club africanais ni wazuri hasa,kumfunga Kipanga goli 7 si kubahatisha..walimfunga kweli...
Na Kipanga kutoa draw kule Znz si kwamba kipanga alishindikana kufungwa bali wale waarabu walichukua muda mwingi kuwasoma kipanga kwa ile 1st leg
Hivyo tusibweteke kabisa na kuchukulia wale walitoa draw na Kipanga ati sisi itakua kazi rahisi tusijidanganye!

Cha kufanya tukaze buti tupambane na kushinda idadi itakayowezekana ya magoli kwa mechi hiyo mkondo wa kwanza...kabla ya kurudiana tarehe 9...
Hiyo ndiyo silaha pekee tuliyonayo na si kuwabeza waarabu.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Yanga ni kubwa sana mwarabu atapigwa kama ngoma,tena hawa waarabu weupe ni laini laini sana
 
Hapa mtaweza kushinda na kusawazisha makosa yenu mliyofanya kwa Al Hilal ,ila changamoto ni kule ugenini

Nimeshuhudia waarabu wakifungwa goli 2-0 ugenini halafu cha ajabu mechi ilivyoisha wao ndio wakawa wanashangilia

Kiukweli sikuwaelewa wanamaana gani mpaka pale nilipokuja kuangalia 2nd leg ambayo walishinda bao 6-0
 
Hawa jamaa tunahitaji kuwafunga magoli Mengi sana hapa nyumbani

Kule kwao wanatumia Nguvu kubwa ya mashabiki Yanga anahitaji kushinda magoli kuanzia 4 na kuendelea hapa nyumbani
 
Utopolo ni wepesi sana kwa hawa jamaa. Wana historia kubwa tu.. walianza 1920, wamechukua CAF champions league cup x 1, ubingwa wa Tunisia x 11 na kombe la FA x13.
 
Hawa jamaa tunahitaji kuwafunga magoli Mengi sana hapa nyumbani

Kule kwao wanatumia Nguvu kubwa ya mashabiki Yanga anahitaji kushinda magoli kuanzia 4 na kuendelea hapa nyumbani
utopolo wakushinda goli bado hajazaliwa, acha kuota utajikojoleaaa
 
Hawa jamaa tunahitaji kuwafunga magoli Mengi sana hapa nyumbani

Kule kwao wanatumia Nguvu kubwa ya mashabiki Yanga anahitaji kushinda magoli kuanzia 4 na kuendelea hapa nyumbani
Hayo magoli manne yatoke wapi wkt Mbuni FC mliwafunga kwa taaabu 2-1.
 
Back
Top Bottom