Yanga tutengeneze mikakati ya kujitegemea na sio kuomba omba

Yanga tutengeneze mikakati ya kujitegemea na sio kuomba omba

Nyankuru Wankuru

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2018
Posts
1,199
Reaction score
1,346
[http://www]

Harambee ya Uchangiaji ndani ya Klabu ya Yanga iliyoendeshwa na Kamati ya Hamasa, imevuna kiasi cha Sh 920 Milioni zikiwa ni fedha taslim na ahadi za wadau mbalimbali wa klabu hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Anthony Mavunde alisema kwa shughuli iliyofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee leo, walikusanya fedha taslimu Sh 263 milioni, huku zile za awali zikiwa Sh252 milioni na fedha hizi zikichanganywa pamoja na ahadi zote zinatoa jumla ya Sh 920 milioni.

[http://www]

Lengo la Kamati hiyo ni kukusanya Sh 1.5 bilioni kwa nia ya kusaidia usajili wa klabu hiyo kwa kikosi cha msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

“Kwa hakika tunajivunia kwa hili lililofanywa na Wanayanga na wale wanaotaka kuendelea kuichangia wanakaribishwa kwa vile Yanga bado inahitaji fedha kwa maendeleo ya klabu hiyo,” alisema Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla.
 
Kujitegemea ni muhimu ila suala kuwa na uwanja binafsi nalo linatakiwa lipewe kipaumbele sana, Kuna kipindi Mwenyekiti Manji alionesha hadi na ramani sijui wameishia wapi, maana ukiwa na uwanja wako na kwa wingi wa mashabiki kama wa timu yetu inakua ni chanzo kizuri cha mapato, kwengineko nasikia wametangaza zabuni kwa ajili ya matumizi ya neno ya Yanga, tabia ya kutengeneza jezi feki na kuzagaa mitaani ikomeshwe, pia tuwetunasajili vijana wadogo wenye vipaji na kuwauza kama Msuva
 
Back
Top Bottom