Yanga, uingiaji huu wa wachezaji uwanjani ni sawa?

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Wakuu, nazipongeza timu zetu kwa matokeo mazuri ya mechi za CAF zilizochezwa hspa nyumbani.
Naomba mnisaidie utaratibu wa timu ya Yanga wachezaji kuingia uwanjani.
Nimezowea kuona timu zinapoingia uwanjani hutanguliza kapteni halafu golikipa kama kipa si kapteni, kwa maana kapteni atangulie.
Sasa kwa Yanga hii ni mechi ya pili kumuona Mayele ambae si kapteni akiongoza wachezaji wenzie kuingia uwanjani. Jana walijipanga vizuri kwa Mwamyeto kutangulia, lakini ghafla kufika uwanjani Mayele akatangulia, hii inakaaje???
 
Hirizi, hirizi, mbeba hirizi.
 
fanya unacho kiwaza ndio hicho
 
NI MAAGIZO YA KAMATI YA UFUNDI( JUJU) Yanga inaamini sana ktk HILO
 
Kwanini usiulize swali la kwanini mchezaji akiwa staaa anakaa nyuma kabisa kuingia kwa baadhi ya Timu?? Afrika hata huko ulaya je ikitokea akawa wa katikati utauliza?
 
Kwahiyo unateseka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…