Yanga vs Al Ahly ni vita leo, Zesco yasonga mbele Ligi ya Mabingwa

Yanga vs Al Ahly ni vita leo, Zesco yasonga mbele Ligi ya Mabingwa

Status
Not open for further replies.

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2013
Posts
338
Reaction score
180
Yanga ahly.jpg

MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga, wako vitani dhidi ya Al Ahly ya Misri katika mchezo wa marudiano wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo wanatafuta ushindi ama sare ya zaidi ya bao moja ili waingie hatua ya makundi.

Wawakilishi hao wa Tanzania wanaingia uwanjani leo hii huku wakitambua kwamba, wawakilishi wengine, Azam, ambao walikuwa na nafasi kubwa ya kusonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho, wamekwishatolewa.

Kwa habari zaidi, soma hapa => Yanga vs Al Ahly ni vita leo, Zesco yasonga mbele Ligi ya Mabingwa | Fikra Pevu
 
Mhhh...mimi ni shabiki wa Simba ila nawaombea yanga wasonge mbele inshaallah.
 
Nimefarijika tu uwepo wa kiungo Niyonzima aliyekosa mchezo uliopita na kumchezesha Boussou kama kiungo mkabaji. Niyonzima anajiamini na bila shaka atamchangamsha sana Kamusoko kwenye kiungo.

Azam wajilaumu wenyewe kwa kuyachezea magoli pale Chamazi mechi ya awali chini uongozi wa nahodha wao John Bocco aliyekosa magoli ya wazi.
 
Hakuna vita yoyote hapo, mtu anapigwa tatu bila anarudi nyumbani maisha yanaendelea!
 
Naamini Mungu Hawaii wala hachelewi kujibu basi naamini Leo yanga itapokea kipigo kitakatifu toka kwa al ahly eeeh Mungu yapokee maombi yangu.
 
Bandiko lako lina neno vita kitu ambacho timu za kitanzania hakuna wanapokuwa ugenini ..azam kashinda home away kalowa je huyu
 
Lazima wachapwe Namsubiri huyo msemaji wao mwenye mdomo Kama chuchunge najua atakuja na sababu billions.
 
Samahani nilichapia mechi itachezwa SAA 2:30 usiku na itaonyeshwa na Azam two na ZBC 2.
 
Wako vitani wapi watu wamechezea nafasi yao..mnatoa sare nyumbani...Leo yanga wafungwe tu... Tena wapigwe goli nyingi maana hawachelewi kusema wamekufa kiume
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom