Yanga vs Alliance Fc

Yanga vs Alliance Fc

Mimi nimewauliza Simba ebu soma vizuri mkuu!!!

Okey nimekuelewa. Uliposema mnalialia nikajua umeniweka kundi moja na bi hindu fc. Hata hivyo hakijaharibika kitu. Next time swali lolote kwa Mbumbumbu FC li direct kwa Msemaji wao sembo au kwa katibu wao Khaligraph Jordan bila kumsahau shabiki wao lialia mr popoma GENTAMYCINE
 
Ile siku dhidi ya Simba ya 0-0 asingetolewa Ajib Simba lazima angelalala
Tumuamini nani? Maana ukitafsiri maelezo ya Mwalimu wa Yanga baada ya mechi kuhusu Ajib, unapata jawabu kwamba asingetolewa huenda Yanga ingefungwa.
 
Ulichosema mkuu ni ukweli usiopingika hata hivyo aliyefanya hayo si Yanga bali ni uongozi wa TFF ambao ni Simba pure kuanzia Rais mpaka Msemaji wake. Walifanya hivyo kwa ajili ya kuibeba Simba ili imalize mapema michezo ya nje ya Kituo chake kwa kushinda then baadae imalizie kiulaini mechi za Dar. Hasa kwa kuwa iliaminiwa kuwa Yanga kwa kipindi hiki ni wabovu hivyo wangefungwa Dar na mikoani. Hata hivyo, Mungu si Mwakalobo wameumbuka.
Teh teh teh Mkuu unamfahamu sana Mwakalobo?
 
Tumuamini nani? Maana ukitafsiri maelezo ya Mwalimu wa Yanga baada ya mechi kuhusu Ajib, unapata jawabu kwamba asingetolewa huenda Yanga ingefungwa.

Haya ni maoni yangu tu, siyo lazima kabisa uyaamini na wala hulazimishwi...Mwalimu naye ana mawazo yake ya kitaaluma na ambayo anaweza kuwa sahihi lakini pia inawezekana asiwe sahihi kwa namna fulani...ndivyo mambo yalivyo...
 
Sembo mtu safi sana...huwa napenda vibwagizo vyake...Sembo kokote ulipo jitokeze bwana....
Hahahaaa. Huwa anakauoga na hasa ukiangalia leo wanacheza na Stand basi hachelewi kuja baada ya mechi tena kuja yake atakuja na tambo nyingi mnooo.

Mtani sembo uko wapi jamaani. 😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom