Yanga vs Azam,Hakuna mbabe!Mpira Wa Nyumbani imebaki ushabiki tu

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Kuna juhudi kubwa na za lazima kuinua mchezo huu hapa nyumbani kwa kuanza na watoto wadogo kabisa wajengewe misingi na mbinu madhubuti ili waje kua tegemeo LA taifa baadae.
Nimeangalia game hii mwanzo mwisho nilichokibaini ni kua bado Kiwango chetu ni tatizo,inafikia mahala unaona timu zote zinzoshiriki Vpl zina kiwango kimoja,kiwango ambacho kama ni speed 180 kph wao wote wanaishia Speed speed 70 na huenda wachezaji ni hawa hawa wanahama hama tu,
Fikiria Striker anaingia Ndani ya 18 zaidi ya Mara mbili yeye na goli ama anakosa goli ama anaanguka....loh
Tatizo kubwa nililoliona ni Ball Control,hili ni tatizo kubwa sana nchini na ndio kisa waweza laumu walimu hapana,walimu wengi ni wazuri Ila ndio hivyo inakua ngumu kufundishika!uwezo wa kuelewa unagota,
Serikali na Tff kupitia program za kukuza vipaji mlitilie umuhimu sana hili,Watoto wajengewe Football skills ikiwa ni pamoja na speed/acculacy na ball control mapema
Natumai baadae tutafurahi baada ya kuanza kuvuna tulichopanda,tuache ushabiki tu bila kuangalia kiwango.Jana tumeshuhudia mechi nyingi za bpl na LA liga, tunataka na sie tufike pale jamani.
 
Mkuu.. Hayo matatizo uliyoyazungumza.. Simba S .C yamekua historia;

1. Kasi ya soka letu ni 240kph.
2. Kuna kiumbe anaitwa kichuya huyu si mpaka aingie kwenye 18 ndo afunge.. huyu jamaa anafunga toka pambe mbalimbali za uwanja.. Mara toka katikati ya uwanja, anapiga kona goli n.k
3. Kuhusu ball control, Simba ndo tunatoa darasa.. Kuna walimu kama mwinyi Kazimoto 'ball dancer', muzamiru yasin, 'le captain' jonas mkude, mo ibrahimu n.k

Mkuu kwanini usubiri mpaka baadae ndo uanze kufurahi?! Karibu sasa Simba S.C kwa furaha ya milele.
 
Watu weweeeeeee wekundu WA msimbazi ni balaa.
 
Wrote wale wale ushabiki huu ndio umetufikisha hapa si mnaona waganda/Zambia/Drc wenzetu?
 
Simba ni timu nzuri illa wanahitaji mshambuliaji mmoja ambaye nafasi mbili goli yaani goal poacher. Hapo watakamilika maana kwa sasa mpira wa simba unaonekana. Illa mavugo na huyo nani sijui wa kutoka ivory cost hapana bado wanakosa magoli sana. Wakipata mshambuliaji mzuri hata kama okwi yaaani itakuwa ni balaa. Msimu huu wazuri illa warekebishe hapo. Yanga naona wapo hoi wachezaji wengi wamechoka na AAzam wanaunda timu.
 
Mim ni mshabik wa simba ila mahaba yako kwa team siyawez
 
Mbona hujaelezea game yenyewe umeishia kutoa maoni yako tuuuuu!!!
 
Mkuu.. Hayo matatizo uliyoyazungumza.. Simba S .C yamekua historia;

1. Kasi ya soka letu ni 240kph.
2. Kuna kiumbe anaitwa kichuya huyu si mpaka aingie kwenye 18 ndo afunge.. huyu jamaa anafunga toka pambe mbalimbali za uwanja.. Mara toka katikati ya uwanja, anapiga kona goli n.k
3. Kuhusu ball control, Simba ndo tunatoa darasa.. Kuna walimu kama mwinyi Kazimoto 'ball dancer', muzamiru yasin, 'le captain' jonas mkude, mo ibrahimu n.k

Mkuu kwanini usubiri mpaka baadae ndo uanze kufurahi?! Karibu sasa Simba S.C kwa furaha ya milele.
Mbwembwe hizi
 
Wrote wale wale ushabiki huu ndio umetufikisha hapa si mnaona waganda/Zambia/Drc wenzetu?
Waganda kundi waliopangwa hata sisi tungequalify.. Dira ya mpira kwa sasa ni Yanga ndio maana vitimu vingine vinacheza kwa kupania sana utafikiria fainal ya world cup... Jana Azam walicheza rafu mbaya sana utafikiria ni timu kutoka syria... Tazama ranks za CAF timu gani inaongoza ukanda wetu..
NB:rafu anazocheza Agrey Morris mechi ijayo washabiki wa Yanga tutaingia uwanjani tumshikishe Adabu. TFF mtazameni huyu mpemba
 
Simba ni timu nzuri illa wanahitaji mshambuliaji mmoja ambaye nafasi mbili goli yaani goal poacher. Hapo watakamilika maana kwa sasa mpira wa simba unaonekana. Illa mavugo na huyo nani sijui wa kutoka ivory cost hapana bado wanakosa magoli sana. Wakipata mshambuliaji mzuri hata kama okwi yaaani itakuwa ni balaa. Msimu huu wazuri illa warekebishe hapo. Yanga naona wapo hoi wachezaji wengi wamechoka na AAzam wanaunda timu.
Azam kama wataendelea kuwakumbatia kina Bocco, wasahau!
Kuhusu simba nakuunga mkono, hao washambuliaji wawili sio kabisa, simba hii inahitaji mtu kama tambwe, ngoma etc!!
 
Mkuu.. Hayo matatizo uliyoyazungumza.. Simba S .C yamekua historia;

1. Kasi ya soka letu ni 240kph.
2. Kuna kiumbe anaitwa kichuya huyu si mpaka aingie kwenye 18 ndo afunge.. huyu jamaa anafunga toka pambe mbalimbali za uwanja.. Mara toka katikati ya uwanja, anapiga kona goli n.k
3. Kuhusu ball control, Simba ndo tunatoa darasa.. Kuna walimu kama mwinyi Kazimoto 'ball dancer', muzamiru yasin, 'le captain' jonas mkude, mo ibrahimu n.k

Mkuu kwanini usubiri mpaka baadae ndo uanze kufurahi?! Karibu sasa Simba S.C kwa furaha ya milele.

Nyie ndiye mnaoua vipaji vya vijana kwa misifa yenu uchwara....Hivi huyo kichuya ana kitu gani cha ziada???!!! Badala ya kumpa moyo aongeze juhudi nyie mnampa misifa ya ovyo kabisa....Kwa mwenenndo huu wa misifa ya hovyo ni dhahiri mpira utamshinda Kichuya...Lt us wait and see.....
 
Mkuu.. Msuva, Mwashiuya,.. n.k wako wapi siku hizi, naona wamepotea kweli hawa vijana? Kipindi wanafanya vyema, mlikua mkiwapa sifa au mnawapa moyo waongeze juhudi?

Kuhusu Kichuya ana kitu gani cha ziada muulize barthez.. [emoji2] [emoji2]

Au ngoja nikupe nukuu ya kocha bora kabisa barani Africa.. Kinah Phiri wa Mbeya City aliyoinena baada ya kuwagonga 2 kavu.
Namnukuu.. "Nilijuwa wazi Kichuya angetufunga ndiyo maana nilimwambia Kabanda na wenzake wawe makini naye, hata msimu uliopita alitufunga bao kama hilo hilo sasa Kabanda alishindwa kumdhibiti hadi nilipomtoa angalau hali ilitulia, yule mtoto ana kasi hivyo unayemkaba unatakiwa kuwa na mbinu za ziada."

Sasa kama wewe utabishana na "gwiji" wa soka barani Africa.. Haya.
Wacha sisi tumpe sifa + gari kwa kazi nzuri anayoifanya.. Nyinyi endeleeni kumtia moyo.

Ngoja nieendelee kusoma magazeti [emoji116]
1476686253651.jpg

1476686289023.jpg

1476686301965.jpg
 
View attachment 419462
View attachment 419463
View attachment 419464

sembo....nimesoma haraka haraka maoni yako kwani nina shughuli Fulani, lakini nikwambie kitu....hiyo misifa ndiyo iliyoua vipaji vya Mwashiuya, Msuva na kadhalika....hata Serengeti boys kama 'baadhi ya viongozi wa serikali' wasingeingilia kati kwa kujitokeza pale ilipopata ushindi dhidi ya Afrika Kusini na nyingine sina shaka tungewatoa wale wakongo...sasa bahati mbaya wale 'viongozi' walipoona ile timu inafanya vizuri wakaanza kujitambulisha nayo kwa kutoa ahadi sijui goli moja sh 500,000 sijui mara goli moja sijui sh milioni moja....sasa wale vijana wakachanganyikiwa ...tukashinda goli 3-2 hapa nyumbani....na wataalamu wa mpira walijua ule ndio ulikuwa mwisho wa Serengeti boys....wanasiasa wakianza kujitambulisha kwa mafanikio ya timu ujue huo ndiyo mwisho wa timu...wanasiasa huwatumia wafanyabiashara wanaoahidi kutoa sijui mihela ili nao baadaye waje wajitambulishe na ushindi wa timu...sasa tuje kwenye mada...huyo Kichuya, sijui, Msuva, sijui Mwashiuya...they are not professionals...bado ni watoto wadogo ambao hawahitaji kubebeshwa sifa uchwara na magazeti na wapenzi au mashabiki uchwara wasiojua saikolojia ya wachezaji wa kwetu....Kulikuwa na Boniface Ambani wa Yanga alifunga magoli akalweshwa misifa ya wanayanga, msimu uliofuatia hakufanya kitu...Simba nao walikuwa na mchezaji mmoja hivi nimesahau jina, alikuwa wa nje nadhani kutoka Burundi, akaleweshwa misifa na hakudumu......Yanga si unaiona sasa, imeleweshwa misifa na magazeti ambayo lengo lake ni la kibiashara sasa kiwango chake ni cha wastani tu kama kilivyo cha Simba na Azam....Azam nao walianza kwa moto na viongozi wake wakawa wanatamba sasa hawana kitu, kilichobaki kwao ni mchezo wa rafu kwa mabeki wake kama Aggrey Morris, Nyoni na wengine ambao kama refa ni makini wangepewa red card mechi ya jana kati ya Yanga na Azam kama ilivyo kwa Yondani.....
 
Azam kama wataendelea kuwakumbatia kina Bocco, wasahau!
Kuhusu simba nakuunga mkono, hao washambuliaji wawili sio kabisa, simba hii inahitaji mtu kama tambwe, ngoma etc!!
magoli yenu ya mkono yaishiee huko huko...usituambukize netball sisi
 
Simba ni chuo cha soka.Aidharauliye simba hupotea.YUKO wapi Singano,Kapombe na Kessy.Simba inafundisha mpira,Yanga inatumia vipaji na kuviua.Msuva alikuwa moto,mwashuya, na Ngasa walipofika yanga wakapotea kisoka.Moja ya sifa ya timu bora ni jinsi inavyopokea vipaji na kuviendeleza.Hivyo wenye vipaji wacheze simba ndipo mlango wakwenda Ulaya utafunguka.
 
sembo....nimesoma haraka haraka maoni yako kwani nina shughuli Fulani, lakini nikwambie kitu....hiyo misifa ndiyo iliyoua vipaji vya Mwashiuya, Msuva na kadhalika....hata Serengeti boys kama 'baadhi ya viongozi wa serikali' wasingeingilia kati kwa kujitokeza pale ilipopata ushindi dhidi ya Afrika Kusini na nyingine sina shaka tungewatoa wale wakongo...sasa bahati mbaya wale 'viongozi' walipoona ile timu inafanya vizuri wakaanza kujitambulisha nayo kwa kutoa ahadi sijui goli moja sh 500,000 sijui mara goli moja sijui sh milioni moja....sasa wale vijana wakachanganyikiwa ...tukashinda goli 3-2 hapa nyumbani....na wataalamu wa mpira walijua ule ndio ulikuwa mwisho wa Serengeti boys....wanasiasa wakianza kujitambulisha kwa mafanikio ya timu ujue huo ndiyo mwisho wa timu...wanasiasa huwatumia wafanyabiashara wanaoahidi kutoa sijui mihela ili nao baadaye waje wajitambulishe na ushindi wa timu...sasa tuje kwenye mada...huyo Kichuya, sijui, Msuva, sijui Mwashiuya...they are not professionals...bado ni watoto wadogo ambao hawahitaji kubebeshwa sifa uchwara na magazeti na wapenzi au mashabiki uchwara wasiojua saikolojia ya wachezaji wa kwetu....Kulikuwa na Boniface Ambani wa Yanga alifunga magoli akalweshwa misifa ya wanayanga, msimu uliofuatia hakufanya kitu...Simba nao walikuwa na mchezaji mmoja hivi nimesahau jina, alikuwa wa nje nadhani kutoka Burundi, akaleweshwa misifa na hakudumu......Yanga si unaiona sasa, imeleweshwa misifa na magazeti ambayo lengo lake ni la kibiashara sasa kiwango chake ni cha wastani tu kama kilivyo cha Simba na Azam....Azam nao walianza kwa moto na viongozi wake wakawa wanatamba sasa hawana kitu, kilichobaki kwao ni mchezo wa rafu kwa mabeki wake kama Aggrey Morris, Nyoni na wengine ambao kama refa ni makini wangepewa red card mechi ya jana kati ya Yanga na Azam kama ilivyo kwa Yondani.....
Nimekuelewa vyema Mkuu.. Nadhani ni akili ya mtu tu.. Kuna wapo vijana ukiwasifia ndo unachochea moto, I mean ni kama umewachagiza, wanafanya vyema zaidi.. Mf. samata na ulimwengu.
Nadhani Kichuya atajifunza toka kwa kina Samata na si Msuva wala Mwashiuya.
 
Ni kweli kuna exceptions....Samatta na Ulimwengu...wana bahati ya kuchukuliwa mapema kutoka hapa nyumbani Tanzania...wale ni professionals na wanaishi ki-professional...kumbuka Samatta na Ulimwengu hawakukaa muda mrefu Simba...vipaji vyao vilionekana na wanaojua mpira wakaondolewa mapema hapa...Lakini huyo Kichuya wenu utakuja kuniambia kama atadumu na mpira huo kama kweli ana mpira...Sembo mimi naifahamu soka, ni bahati mbaya siwezi kusema mengi hapa kuhusu soka ya Tanzania....nakuthibitishia kuwa kwa soka ya Tanzania mimi ni 'authority' wa namna yake...najua saikolojia ya wachezaji, nawafahamu...nawafahamu mashabiki wa Tanzania na viongozi wake...nimefanya research na kuwa mmoja wa wanafamilia wa soka ya Tanzania na uongozi wake..I know what I am talking about...Soka ya Tanzania inauawawa na mambo mengi.: moja ni leadership (uongozi wa soka wa Tanzania ni wa ovyo kupindukia kama ilivyo kwa viongozi wa taasisi mbalimbali). Pili, ni jamii yenyewe ya Watanzania ambayo haijitambui kwa mambo mengi. watu wanalalamika kuwa soka ya Tanzania ipo chini lakini wanashindwa kujiuliza ni jambo gani watanzania tumefanikiwa? maendeleo ya soka ya Tanzania huwezi kuyatenganisha na hali halisi ya masuala mengine nchini kama ya kisiasa, kiuchumi, kibiaashara na kadhalika...tatu ni corruption...Soka ya Tanzania imegubikwa na corruption ya kutisha..matokeo mengi hupangwa..Hili siwezi kuliongelea kwani linagusa wengi...Ndugu yangu sembo ukifahamu kiwango cha rushwa katika soka ya Tanzania kilivyo unaweza hata usiende kuhudhuria mechi zinazochezwa kwenye ligi...Lakini corruption haiko kwenye soka tu ipo pia katika maeneo mengine nchini...Corruption katika soka inagusa mpaka kwenye uchaguzi wa viongozi na kadhalika...naona naongea mengi ngoja niishie hapa....Lakini ukiona baadhi ya klabu kubwa nchini zinahadaiwa mpaka kutaka 'kukodisha' au kuuza klabu zao na kusahau hata mambo mengi ya nyuma na historia ya klabu ndipo ujue ukubwa wa tatizo lilipo...yaani wafuasi na wanachama wa klabu nchini ni wa 'mwendokasi' au dot.com hawawezi kufikiri au kuchambua mambo... wakilipiwa ada ya uanachama na kupewa pilau kwenye mikutano huwaambii kitu...ni hatari...
 
Shikamoo Mkuu 1954.. Nimekuelewa vyema sana.. Ila hivi ni nani aliwaza au hata kufikiri kua yule Samata wa Africa Lyon leo atakua ubeligiji??
Kwa hili la kichuya tumpe mda na si kumhukumu mapema kua hatafika popote.
 
Back
Top Bottom