Kamati ya bodi ya ligi imeifuta Kadi nyekundu aliyopewa nahodha wa Simba, Jonas Mkude baada ya kuthibitika hakustahili kadi hiyo.
Pia imeipiga faini ya milioni 5 klabu ya simba na kulipa gharama za uharibifu wa viti uliofanywa na washabiki wake katika mchezo wa Yanga na Simba.
Kamati inaendelea na uchunguzi kuhusu uchezeshaji wa mwamuzi wa mechi hiyo, Martin Saanya na wasaidizi wake, Samwel Mpenzi na Ferdinand Chacha kabla ya kutangaza uamuzi wake.
Ofisa habari wa Simba, Haji Manara naye amelimwa 200,000 kwa kuingia uwanjani baada ya mechi hiyo ilhali hakuwa miongoni mwa maofisa wa mechi waliotakiwa kuwepo katika eneo hilo.
Klabu ya Azam imepigwa faini ya milioni tatu kwa kuvaa nembo ya mdhamini kwenye mkono mmoja badala ya miwili kinyume cha kanuni, JKT Ruvu imwpewa onyo na faini ya laki tano.
Mwamuzi Ahmed Seif amefungiwa miezi sita kwa kushindwa kumudu mchezo wa African Lyon na Mbao FC.