Yanga Vs Simba: Kadi nyekundu ya Jonas Mkude yafutwa, Simba yalimwa milioni 5

Casuist

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2014
Posts
1,189
Reaction score
2,970
Kamati ya bodi ya ligi imeifuta Kadi nyekundu aliyopewa nahodha wa Simba, Jonas Mkude baada ya kuthibitika hakustahili kadi hiyo.

Pia imeipiga faini ya milioni 5 klabu ya simba na kulipa gharama za uharibifu wa viti uliofanywa na washabiki wake katika mchezo wa Yanga na Simba.

Kamati inaendelea na uchunguzi kuhusu uchezeshaji wa mwamuzi wa mechi hiyo, Martin Saanya na wasaidizi wake, Samwel Mpenzi na Ferdinand Chacha kabla ya kutangaza uamuzi wake.

Ofisa habari wa Simba, Haji Manara naye amelimwa 200,000 kwa kuingia uwanjani baada ya mechi hiyo ilhali hakuwa miongoni mwa maofisa wa mechi waliotakiwa kuwepo katika eneo hilo.

Klabu ya Azam imepigwa faini ya milioni tatu kwa kuvaa nembo ya mdhamini kwenye mkono mmoja badala ya miwili kinyume cha kanuni, JKT Ruvu imwpewa onyo na faini ya laki tano.

Mwamuzi Ahmed Seif amefungiwa miezi sita kwa kushindwa kumudu mchezo wa African Lyon na Mbao FC.

 
Kamati ya bodi ya ligi imeifuta Kadi nyekundu aliyopewa nahodha wa Simba, Jonas Mkude baada ya kuthibitika hakustahili kadi hiyo.

Pia imeipiga faini ya milioni 5 klabu ya simba na kulipa gharama za uharibifu.
Source kamanda
 
Kamati ya Bodi ya Ligi ya Uendeshaji leo imetoa adhabu kwa vilabu kadhaa nchini kutokana na makosa mbalimbali, ikiwemo klabu ya Simba iliyotozwa faini ya Shilingi milioni 5 kufuatia mashabiki wake kung’oa viti katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya watani wao Yanga uliopigwa Oktoba Mosi, katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.

Faini hiyo inakwenda sambamba na gharama zingine ambazo klabu hiyo itatakiwa kuingia katika kufidia uharibifu uliofanywa na mashabiki wake.

Ifuatayo ni barua ya TFF ikielezea mchanganuo wa adhabu hizo kwa vilabu mbalimbali.


Chanzo: Hivi Sasa

 
Inasemekana ile haikuwa kona bali ulikuwa mpira wa kurushwa tatizo kale katoto kaliuweka mpira kwenye kisahani cha kona na kichuya akipiga na msaidizi wa refa hakumwambia arushe! Ila binafsi bao Tambwe ni goli sahihi na nimoja ya magoli mazuri kuwahi kufungwa kwenye ardhi ya Tanzania!
 
Ile ilikuwa kadi halali tatizo TZ tunapenda kubebana sana! Hata Simbwa wote wanajua ilikuwa ni kadi halali tena yakujitakiwa nahodha mzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…