Jezi mpya za Yanga kwaajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika zimeandikwa Visit Zanzibar kwa nyuma upande wa chini.
Huko ni kujipendekeza kiwango cha SGR.
Kwanini wasitangaze Visit Tanzania, Visit Mount Kilimanjaro, Visit Ngorongoro, Visit Tarangire au basi Visit Kigoma na maeneo mengine ya utalii yanayopatikana Tanzania bara?
Ninavyojua Zanzibar wana timu zao na wanapaswa kujitangaza wao.
Viongozi Yanga hasa mnaojiandaa kugombea ubunge mwakani acheni kujipendekeza huko Zanzibar! Huo ni uchawa