Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Tangu Rais Mama Samia Suluhu Hassan atangaze motisha ya shilingi milioni tano kwa kila goli litakalofungwa na Simba au Yanga kwenye michuano ya kimataifa, Yanga wamekuwa watu wa 'kutaka sifa'. Wamekuwa wakichota mamilioni kwenye kila mchezo.
Wakati watani zetu Simba hadi sasa wakipata milioni kumi kwa magoli mawili ya mechi mbili za Vipers, Yanga wameshatia kibindoni milioni thelathini kwa magoli sita dhidi ya Mazembe na Real Bamako. Yanga wanaelekea kumaliza kibubu cha ahadi tamu ya Mama Samia.
Natoa wito wa kuwadhibiti Yanga ili wapunguze sifa za kuvuna mamilioni ya Mama. Na naomba, ili watani zetu nao wapate chochote kitu, ahadi hii itumike pia kwa ligi ya ndani ambapo Simba aka Mnyama anaongoza kwa kufunga magoli mengi.
Wapi Baleke? Wapi Bocco? Wapi Chama? Wapi General Phiri? Wapi Sakho?