Yanga wagomea kuvaa jezi zenye nembo ya mdhamini wa ligi NBC mechi ya KMC

kasenene

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2008
Posts
1,632
Reaction score
2,413
Katika mechi yao leo na KMC. Yanga wamevaa jezi isiyokuwa na nembo ya ya mdhamini tofauti na timu nyingine kama tulivyoona katika mechi nyingine zilichezwa leo.

Wadau wengi wa soka tunasubiri kusikia kauli ya TFF. Kwani hili ni tukio kubwa saana kwa mustakabari wa soka letu.

Kuna mtu kaniuma sikio kuwa wanastahili kunyan'gaywa point mbili na goli mbili ahaaa
 
Katiba ya yanga inakataa matumizi ya nembo yoyote yenye rangi nyekundu…………..!
 
We jamaa inaonekana hujui lolote katika soka, kwenye mpira wa miguu hakuna pointi mbili na Tff hawana ubavu wa kunyang'anya Yanga point yoyote.
 
Kwa nini unateseka? Kulikoni kwani?
 
Mchawi mkuu wa maendeleo ya soka la Bongo ni uswahili na ujuaji wa Simba na Yanga
 
Wabaki na point moja na goli zero

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Walishawaambia TFF kuwa jezi walinunua kabla mdhamini hajapatikana na hawana pesa ya kununua nyingine
 
Mdhamini ndo msemaji wa mwisho, timua hao nyang'au wasambaratike wapoteane kama genge la kunguni limeona mwanga
 
Uto ni washamba tu, wangeanza kwanza kuwakataza wachezaji wao kuvaa viatu vyenge rangi nyekundu wakati wa mechi.
 
Yanga kwenye mpira wa miguu wa nchi hii hapangiwi masharti, Kama mdhamini ana masharti dhidi ya Yanga aka anzishe Ligi yake. Yanga ndiye mwenye mpira wake.
 
Mdhamini ndo msemaji wa mwisho, timua hao nyang'au wasambaratike wapoteane kama genge la kunguni limeona mwanga
Yanga ni timu ya Wananchi! Na hivyo itaendelea kubakia kuwa mali ya Wananchi!

Huyo Mdhamini hana ubavu wa kuifanya Yanga chochote! Hivyo acha kujiongezea presha ndani ya mwili wako. Maana utakufa kabka ya wakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…