Yanga wakianza na Kikosi hiki matokeo ni lazima

Yanga wakianza na Kikosi hiki matokeo ni lazima

- Namba 1 Diara

- Namba 2 Kibwana

- Namba 3 Job

- Namba 4 Bacca

- Namba 5 Bakari

- Namba 6 Bangala

Namba 7 lomalisa. Namuweka lomalisa hapa kwa sababu mechi hii inahitaji watu ambao wanajua kupiga dribble vizuri ili kupenyeza mipira kwenda kwa Mayele kutokana na kukajaa kwa mabeki wa USM Alger nyuma leo hawatawapa Yanga nafasi ya kukimbia na mpira sana.

Kwa hiyo kunahitajika mtu ambaye anajua ku dribble, kucheza hapa Moloko na Kisinda sio wazuri kwa dribble.

- Namba 8 Djuma Shaban. Kwa Juma Shabani naye ni hivyo hivy, nafikiri hapa panamtosha. Hata kama sio sehemu sahihi yake ya kucheza, ila kwasababu ya utulivu wake na dribble zake anaweza kuwa anatoa pasi nzuri akiwa hapa.

-Namba 9 Mayele

- Namba 10 Musonda

- Namba 11 Morrison
Hii nchi sasa uhuru umezidi.
 
Tatizo kubwa kwa Yanga ni mabeki kwani kuna wakati wanapwaya sana na hii ndio itawaua na leo pia.

Vilevile kipa Diarra anakuwa na mchecheto wa kutoka golini mara kwa mara timu inaposhambuliwa hali ambayo inafanya kufungwa inakuwa rahisi sana.

Aziz Ki asicheze kwani amekuwa mbovu sana kwa sasa na anapoteza sana mipira.
 
MPIRA una MATOKEO Matatu.

YANGA Lazima wapate
Kufunga
KUFUNGWA
SARE.

HII SI MECHI YA MAJARIBIO KWA WACHEZAJI HII NI FAINALI.

Tangu lini JUMA Shaban akacheza 8
Hiyo pumzi ya kiuongo unajijua unaisikia.
Huyo Romalisa tangu lini akacheza No 7
Angalau ungesema 11.

Job Leo hawezi kuwepo,
ANATUMIKIA ADHABU ya Kadi.

KWANZA HUJUI MPIRA
 
Back
Top Bottom