Yanga wakisikia Ateba na Mukwala wanapata kiwewe kuelekea Machi 08

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
1741265146925.png
Mastaa wawili kwenye eneo la ushambuliaji ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu,Fadlu Davids ngoma ni nzito kutokana na kuliamsha dude kwenye eneo la ufungaji katika mechi ambazo wamechza.

Ni Machi 8 2025 Uwanja wa Mkapa unatarajiwa kuwa kazini kwa wababe wawili Yanga na Simba kukutana uwanjani kwenye msako wa pointi tatu huku Yanga katika eneo la ushambuliaji wakiwa na rekodi bora Simba wakifuata.

Ni mabao 58 safu ya ushambuliaji ya Yanga imetupia huku ile ya Simba ikiwa na mabao 46 baada ya kucheza jumla ya mechi 21 na Yanga ni mechi 22 imecheza msimu wa 2024/25 ambao ushindani wake ni mkubwa mwanzo mwisho.

Ateba ni dakika 1,117 kakomba uwanjani akifunga mabao 8 na pasi tatu za mabao katika mechi 17 ambazo alipata nafasi huku Mukwala akiwa amecheza jumla ya mechi 19 akikomba dakika 666 akifunga mabao 8 na pasi mbili za mabao.

Taarifa zinaeleza kuwa kwa sasa ndani ya Simba kwenye benchi la ufundi hesabu kubwa ni kujua nani ataanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo ujao kutokana na uimara wa wachezaji hao kwenye kucheka na nyavu kuwa sawa kirekodi.

“Kariakoo Dabi inamengi na miongoni mwa hay oni eneo la ushambuliaji bado haijajulikana nani ataanza kikosi cha kwanza kwenye eneo la ushambuliaji kati ya Ateba ama Mukwala, lakini hili sio baya kwa kuwa wote ni wachezaji wa Simba benchi la ufundi litaamua.” Ilieleza taarifa hiyo.
 
Nchi hii ina mambo ya ajabu kwenye mpira wa miguu, yaani timu ina Ateba, Mukwala na Kibu na wameshupaza Shingo wanataka ubingwa!!!
Hii ndio inapelekea Marefa kudhallika ikwa kupindisha sheria za soka kumfurahisha aliyewapa maelekezo.

Timu iliyostahili kushika nafasi ya nne ina bebwa kuwa nafasi ya pili
 
Ndugu yangu Mimi ni simba mwenzio
Timu yetu ina Changamoto nyingi sana Ila Pia haina mshambuliaji hata mmoja wa Maana

Angalau simba ingekuwa na mshambuliaji mwenye Daraja A Africa angalau kama.
1. Fiston Mayele.
2. Agostinho Cristóvão Paciência (Mabululu).
3. Jonathan sower.
Nk.

Sio hao wachezaji wa Daraja C
 
Mastaa wawili kwenye eneo la ushambuliaji ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu,Fadlu Davids ngoma ni nzito kutokana na kuliamsha dude kwenye eneo la ufungaji katika mechi ambazo wamechza.

Ni Machi 8 2025 Uwanja wa Mkapa unatarajiwa kuwa kazini kwa wababe wawili Yanga na Simba kukutana uwanjani kwenye msako wa pointi tatu huku Yanga katika eneo la ushambuliaji wakiwa na rekodi bora Simba wakifuata.

Ni mabao 58 safu ya ushambuliaji ya Yanga imetupia huku ile ya Simba ikiwa na mabao 46 baada ya kucheza jumla ya mechi 21 na Yanga ni mechi 22 imecheza msimu wa 2024/25 ambao ushindani wake ni mkubwa mwanzo mwisho.

Ateba ni dakika 1,117 kakomba uwanjani akifunga mabao 8 na pasi tatu za mabao katika mechi 17 ambazo alipata nafasi huku Mukwala akiwa amecheza jumla ya mechi 19 akikomba dakika 666 akifunga mabao 8 na pasi mbili za mabao.

Taarifa zinaeleza kuwa kwa sasa ndani ya Simba kwenye benchi la ufundi hesabu kubwa ni kujua nani ataanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo ujao kutokana na uimara wa wachezaji hao kwenye kucheka na nyavu kuwa sawa kirekodi.

“Kariakoo Dabi inamengi na miongoni mwa hay oni eneo la ushambuliaji bado haijajulikana nani ataanza kikosi cha kwanza kwenye eneo la ushambuliaji kati ya Ateba ama Mukwala, lakini hili sio baya kwa kuwa wote ni wachezaji wa Simba benchi la ufundi litaamua.” Ilieleza taarifa hiyo.
Nataman kocha apange washambuliaji wawili
 
Back
Top Bottom