Yanga walalamika Simba kuongezewa dakika nyingi katika mechi

Yanga walalamika Simba kuongezewa dakika nyingi katika mechi

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Kupitia Mkutano na waandishi leo Februari 8, 2022, Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amezitaja takwimu ambazo zinaonesha kuwa na utata katika kuweka usawa kwenye timu ya Yanga dhidi ya wapinzani wao, Simba.

Moja ya Takwimu ambayo ameitaja ya kwanza ni Dakika za Nyongeza ambazo hutolewa mwishoni mwa mchezo.

Bumbuli amesema kuwa katika michezo 14 ambayo Klabu ya Young Africans ilicheza kwenye Ligi Kuu msimu huu, walibahatika kuongezewa dakika 34 tu (Jumla) ikiwa na mgawanyiko wa ongezeko la dakika 2, 3 mpaka 5.

Kwenye michezo 15 ambayo Klabu ya Simba iliyocheza kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu, waliongezewa dakika 75 ikiwa na mgawanyiko wa ongezeko la akika 4, 5 mpaka 7.

WhatsApp-Image-2021-09-08-at-12.46.11-PM-1-950x633.jpg
 
Mbona jina la aliepo pichani na jina la kwenye habari ni tofauti ama Manara anatumia majina mawili ?
 
Hivi utopolo wakiwa wanaongoza na mechi ikiongezwa DK chache ni Nani wa kulalamika?

Mambo mengine ni aibu kwa kweli.
 
Kwa anataka dakika ziongezwe kwa usawa bila kujali muda uliopotea?
Malalamiko FC wameshaanza
Wangefungwa na Mbeya City sijui ingekuwaje
 
Achana na paka shume huyo, juzi hapo na mbeya city wameenda halftime dakika ya 51

Halafu wameanza kipindi cha pili dakika 45, baada ya hapo tena zikaongezwa zingine halafu anakija pumbuli kutapika nyongo kwamba simba inapendelewa
 
Back
Top Bottom