Yanga wamelewa sifa?

Kyachakiche

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2009
Posts
986
Reaction score
208
Tangu timu ya Yanga walipochukua ubingwa wa Tz bara kwa mara ya pili mfulilizo, tumekuwa tunashuhudia ama kusikia kauli mbalimbali kutoka kwa viongozi wake. Kwa mfano M/Kiti wake Ndg Madega alisikika akisema kuwa huenda ligi inayokuja ikachezwa kwenye uwanja wao wa Kaunda na kwamba wao ni viongozi makini ambao hawakurupuki kwani ni timu kubwa. Tumemsikia pia coach wao Condic akisema hamwitaji Juma Kaseja kwani hakuwa msaada sana kwa timu hivyo anamfungulia mlango wa kutokea. Wachezaji wengine mahiri kama Nsajigwa,Ambani, Owino, Sunguti, Cannavaro,nk, wako mguu nje mguu ndani. Kwenye usajili unaoendelea hatusikii saana mikakati yao kama zilivyo timu nyingine huku wakiwa ndio wawakilishi wetu wa ligi mabingwa wa Africa hapo mwakani. Mimi nawauliza wanaJF wenzangu, Je, huku si kulewa sifa ya kuchukua ubingwa wa Tz mwaka huu wakiwa na mechi kadhaa mkononi na kudhani kwamba wao ni wao tu hata huko tuendako?
 
Tff wameshasema kuwa mwaka huu yanga hawatasajili maana hawawezi kuacha mchezaji muda umeshapita....wajua kuna wajuanji wanjinga sana pale kuanzia madega na wenzake...walitaka simba waanze ili wasije wakawapa mwanya simba kuiba kina ambani jamani mchezaji yule mwaka huu si wenu tenaa wenzetu wanakuja tafuta channel duu sio waje wazeekee hapa tz...ehh waacheni waende zao
 
Mkuu tuko pamoja kwenye hili!
 
Wadau si kwamba nawarejesha nyuma. Nilikuwa napitia baadhi ya mabandiko ya zama kidogo nikaja kukutana na utabiri huu. Je, ni kweli mawazo yaliyokuwa kwenye hii mada yanaweza kuwa ya kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…