Kyachakiche
JF-Expert Member
- Feb 16, 2009
- 986
- 208
Tangu timu ya Yanga walipochukua ubingwa wa Tz bara kwa mara ya pili mfulilizo, tumekuwa tunashuhudia ama kusikia kauli mbalimbali kutoka kwa viongozi wake. Kwa mfano M/Kiti wake Ndg Madega alisikika akisema kuwa huenda ligi inayokuja ikachezwa kwenye uwanja wao wa Kaunda na kwamba wao ni viongozi makini ambao hawakurupuki kwani ni timu kubwa. Tumemsikia pia coach wao Condic akisema hamwitaji Juma Kaseja kwani hakuwa msaada sana kwa timu hivyo anamfungulia mlango wa kutokea. Wachezaji wengine mahiri kama Nsajigwa,Ambani, Owino, Sunguti, Cannavaro,nk, wako mguu nje mguu ndani. Kwenye usajili unaoendelea hatusikii saana mikakati yao kama zilivyo timu nyingine huku wakiwa ndio wawakilishi wetu wa ligi mabingwa wa Africa hapo mwakani. Mimi nawauliza wanaJF wenzangu, Je, huku si kulewa sifa ya kuchukua ubingwa wa Tz mwaka huu wakiwa na mechi kadhaa mkononi na kudhani kwamba wao ni wao tu hata huko tuendako?