Yanga wana Mwanasheria kweli?

Yanga wana Mwanasheria kweli?

Habari za ijumaa wapenzi na mashabiki wa soka nchini Tanzania pamoja na afrika mashariki.

Ikiwa yamepita masaa machache toka kutambulishwa kwa mchezaji aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mpira Tanzania huku hali ikiwa shwari pale jangwani baada ya kuwa na uhakika wa usajili wa Ki Aziz licha ya changamoto mbali zilizojitokeza katika kukamilisha dili hilo.

Sasa twende kwenye mada muhimu:‐

Ukiangalia baadhi ya mambo yanavyoendeshwa pale jangwani kuna vitu vinashangaza sana swali la kujiuliza kila shabiki na mpenda soka kwa sasa nchini Tanzania ni kweli yanga wana mwanasheria?
Mbona mambo yao wanafanya kama team ya ndondo cup maana ni ya kukurupuka tu kwa mfano,

Sakata la Morrison lilivyokuwa kabla hajaenda simba tuliaminishwa kuwa Morrison aliongeza mkataba baada ya ule wa awali kuisha na picha zilisambaa mitandaoni zikimuonyesha akiwa na mwenyekiti wa kipindi hcho kwenye kochi lile lile analotumia kumsainisha kila mchezaji ila mwisho, wa siku taarifa zilikuwa za uongo na picha zilikuwa danganya toto tu hakuna mkataba wowote uliosainiwa na mwisho wa siku Morrison alienda upande wa pili na kesi baadae ilitolewa maamuzi na Morrison alishinda na kulipwa fidia kweli yanga wana mwanasheria?

Kisa cha pili ni sakata jipya lililoibuka la kuahirisha kambi nchini uturuki ambayo ilitarajiwa kuanza kufanyika kuanzia tar 15/07/2022 mpaka tar 04/08/2022 ambapo kutokana na sababu zisizo julikana yanga wamesitisha kuweka kambi nchini humo wakati huo walishafanya bookings ,
na sehemu waliyoiandaa kufika katika kipindi chote watakachokua huko na baadae wametakiwa kulipa hela za kitanzania Million 200 kama fidia na usumbufu waliosababisha na bookings waliyofanya kabla kweli yanga ndugu zangu wana mwanasheria?

Sakata la tatu kwenye mechi ya CAF champion's league iliyofanyika Benjamin William mkapa yanga walipewa taarifa kuwa wasiingie mashabiki katika mechi hyo kutokanaila na sheria za Covid–19 badala yake mechi ilipofika mashabiki walikuwepo uwanjani na CAF kuwapiga faini ya, dola 5,000 pamoja na onyo kali baada ya kuwafanyia vurugu viongozi na baadhi ya wachezaji wa Rivers United walipokuja kucheza Tanzania ni kweli yanga wana mwanasheria halafu wanataka kufika mbali CAF si watafilisika kwa faini maana inaonekana hata mikataba wanayosaini wachezaji wake ina shida sema tu ni vile wachezaji wetu wazawa walikimbia umande.

NB: Msipobadilika mtafilisika kwa faini tafuteni mwanasheria mzuri kama yasmin yule wa msuva nawakumbusha tu maana CAF champion's league inaanza muda si mrefu.
Acha bangi wewe unaweza kuthibitisha icho cha kambi ya uturuki? Unao ushahidi wa icho unachokieleza? Kurukia rukia mambo usiyoyajua kutakuja kukuingiza matatizoni siku moja kuwa makini na ujinga wako tunakuonya
 
Hivi kuna mtanzania mjinga kushinda manara Tanzania kwa umri wake na ujinga anaopost haviendani kamuelimishe yule kwanza na wale wanaoenda airport kuwapokea wageni wakielewa uje unieleweshe na mimi sawa utopolo.
 
Kuna mbumbumbu mwenzao anaitwa Jemedari Said, from nowhere tu ameamua kuwajaza upepo, na wenyewe wamejaa.
Kwani si hata habari ya manara kugombana na raisi karia aliileta jemedari mwisho wa siku muhusika aliomba msamaha licha ya kukataa awali .
 
Kwa taarifa yako mwanasheria wa yanga anaitwa Simon, ni mtanzania pekee kuwahi kuteuliwa kuwa. Wakili wa mahakama ya ICC, ......mbali na hapo nikwambie tu acha roho mbaya
 
Kwa taarifa yako mwanasheria wa yanga anaitwa Simon, ni mtanzania pekee kuwahi kuteuliwa kuwa. Wakili wa mahakama ya ICC, ......mbali na hapo nikwambie tu acha roho mbaya
Kazi ni connection hata afanye kazi ikulu atakuwa kilaza tu hawezi shindwa kujua vitu vidogo vidogo kama hvyo anaacha team inapigwa faini kila siku kama mwanasheria hayupo
 
Wakili wa yanga ni Simon Patrick amekula shavu huko ICC wakili wenu si alikuwa Morrison?😂😂
 
Kazi ni connection hata afanye kazi ikulu atakuwa kilaza tu hawezi shindwa kujua vitu vidogo vidogo kama hvyo anaacha team inapigwa faini kila siku kama mwanasheria hayupo
Kiufupi unateseka.
Kunywa mo extra lile bomu ufe basi hatuna cha kukusaidia..
 
Hivi kuna mtanzania mjinga kushinda manara Tanzania kwa umri wake na ujinga anaopost haviendani kamuelimishe yule kwanza na wale wanaoenda airport kuwapokea wageni wakielewa uje unieleweshe na mimi sawa utopolo.
Okay, Nenda mahakamani basi kawasilishe malalamiko yako wewe na poyoyo mwenzako uyo jemedari saidi maana sisi atuna msaada kwako, Unamaliza bando kutuletea umbea wa kwenye vijiwe vya kahawa hapa, Rage alikuwa sahihi kumbe aliwaona mapema vichwa vyenu
 
Kwani hujui kama mambo yao yote ni utopolo utopolo
 
Back
Top Bottom