Yanga wanaishukuru Yanga tv

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Nilikuwa miongoni mwa watu wanaorushwa roho kwenye you tube na mitandao mingine nikitafuta habari za kweli za Yanga. "Wahuni" walikuwa wanabandika picha nyingine, maandishi mengine na habari tofauti kabisa, au wanatoa habari za tetesi za kijinga kabisa zilikuwa zinamaliza bundle langu bure. Sasa hv sihangaiki tena na ujanjaujanja ule, kama habari ya Yanga haiko Yanga tv ninaipuuza, sio ya kweli ni uzushi na upuuzi. Binafsi mmenisaidia kuacha kudanganywa na vichwa vya habari vya habari feki

Hongereni yanga tv kwa kuokoa pesa zetu na muda, chapeni kazi.
 
Hakuna binadamu ambaye Hana shauku (curiosity).....hutaacha kupitia hiyo mitandao hata mara moja....
 
Sasa yanga waishukuru au wewe unaishukuru Yanga Tv
Yanga ni mkusanyiko wa vitu, mambo na watu wengi, ila yanga tv ni kitu kimoja tu ndani ya yanga complex. Hivyo ukisema yanga waishukuru Yanga tv unamaanisha watu (wanachama, mashabiki, viongozi, tff, watani wa jadi, nk). Ukiona habari kuhusu yanga haipo Yanga tv, Yanga instagram au yanga App achana nayo kabisa, ni uzushi, ni tetesi ni upigani, ni upotoshaji na njaa kali. Achana nayo kuepuka usumbufu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…