Yanga wanaizungumzia Yanga, Simba wanaizungumzia Yanga

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
MASHABIKI WA SIMBA SC MKO WAPI?

Yanga wanaizungumzia Yanga na Simba wanaizungumzia Yanga.

WanaYanga wameonesha kuumizwa sana kwa Yanga yao kutolewa.

WanaSimba wanaonesha kufurahi sana na hata kukejeli kwa Yanga kutolewa.

Sijaona mwanaSimba anayeonesha kuumizwa na kutolewa kwa Simba, labda wamezoea.

Sijaona MwanaYanga anayeonesha kufurahia kutolewa kwa Simba, kwao sio kitu muhimu.

Dalili zilionekana hata kabla ya mechi ya kwanza, wote mkawa mnazungumzia mechi moja; Young Africans Sports Club vs Mamelodi Sundowns FC
Yanga wakaambiwa wataoga magoli
Video za Masandawana zikasambaa
Mashabiki wa Simba, KMC, Ihefu na wote waliowahi kupigwa goli 5 na Yanga, wakawa mashabiki wa Mamelodi.
Lakini Simba haijaaibika,
Kufungwa nyumbani si aibu,
Kufungwa tena mechi ya marudiano si aibu, Ndio maana mashabiki hawazungumzi chochote.

Mlisema Al Ahly ya msimu huu ni mbovu, wakawafunga nje ndani, nayo hio sio aibu kwenu.

Wanyakyusa tuna msemo unasema;
"Japo wametufunga lakini chenga tumewala!"
Najiuliza; Mtoto wako akileta matokeo mabovu ya mtihani huku akiwa na furaha usoni, kisa eti mtoto wa jirani amefeli, huyo mtoto utambadilisha na ng'ombe au ng'uruwe?

Je hii kitaalamu inaitwaje?
Nawasilisha!
 
Huku kunaitwa kuweweseka....kwa kifupi Simba tumeshapoteana,sioni dalili ya kubeba taji lolote mwaka huu!!
 
Na jezi za Masandawana zikauzwa hatari kwa wapenzi wa timu zilizowahi fungwa 5 na Yanga ikiwemo 5imba
 

Attachments

  • 1712904068956.gif
    42 bytes · Views: 2
  • 1712904069189.gif
    42 bytes · Views: 2
  • 1712904069403.gif
    42 bytes · Views: 2
  • 1712904069597.gif
    42 bytes · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…