YANGA WANAPOKUJA NA PROPOGANDA, UZUSHI NA MBINU ZA KIZAMANI

YANGA WANAPOKUJA NA PROPOGANDA, UZUSHI NA MBINU ZA KIZAMANI

Mohamed Mbelwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
507
Reaction score
272
Akizungumza na Moja ya Wahariri wazuri wa soka, Muhariri huyu ametanabaisha kuwa.


Yanga wameamua kupambana na Simba nje ya uwanja kuliko uwanjani. Na wameamua hawataki tena kuzungumzia ubora wa wachezaji au timu kwa ujumla.
Wanajificha kwenye kivuli kwamba Simba inabebwa au inatumia mbinu chafu kushinda mechi.
Na hili halifanyiki kwa bahati mbaya la hasha.
Ni mpango mkakati uliotengenezawa ila kuharibu mafanikio ya Simba yaonekane ni ya bandia.
Niliwahi kusema na ninarudia Yanga kwa kuzusha jambo lao na kulitengenezea propiganda na wakalishikia bango wamewaacha mbali mno mashabiki wa Simba.
Yanga wana uwezo mkubwa mno wa kuugeuza uongo ukafanana na ukweli.
Wana uwezo wa kuunda kitengo maalum cha propaganda na wakatengeneza njia yao ya kuzusha jambo na wakalisimamia ilimradi wafanikishe lengo lao.
Isivyo bahati mashabiki wa Simba wao hutembea kwenye fact na hoja zenye mashiko na ni wepesi kudharau uzushi na kuachana nao. Hii hupelekea kuonekana wanyonge kwenye mambo ya kuzusha.
Yanga wanayafanya haya kwa manufaa yafutayo.
1. Kuwatafutia mashabiki wao furaha ya bandia.
2. Kuondoa uhalisia wa ubora wa Simba ili ionekane ni timu ya kawaida kama ilivyo yao.
3. Wanajua kelele zao zitawaogopesha marefa na wakichezesha mpira wataogopa na kujaribu kujiondoa kwenye mtego kwamba wanaipendelea Simba. Na hili wanajua litawanufaisha wao.
4. Wanajaribu kuwaogopesha viongozi wote wa mpira waogipe na wafanye vitu kwa woga ili watumie mwanya huo kujinufaisha.
5. Wanajua Simba imewaacha mbali katika msimamo wa ligi hivyo wanatafuta huruma ya maamuzi ili waitumie huruma hiyo angalau kujaribu kujipatia chochote.

Simba inatakiwa ing'amue mbinu hizi na kuanza kuzifanyia kazi mapema. Huu ndio wakati wa wachezaji wa Simba kujituma na kujitolea kila walichonacho ili kuhakikisha wanawafumba midomo wale wote wasiowatakia mema.
Sasa hivi wakipata nafasi ya kumtandika mtu nyingi hakuna mzaha tena ni kuchapa tu kwa idadi kubwa ya magoli kadri itakavyowezekana. Tuwaache wao wachonge midomo sisi tuwajibu kwa vitendo.

Embu tujiulize ni kwa nini hizi lugha za kukatishana tamaa zimeibuka kipindi hiki?
Ni kwa nini kauli ya Manara kwamba Simba itachukua back to back Mara kumi inahojiwa sasa na si wakati alitamka? Ni kwa nini mapungufu ya waamuzi wa Tanzania yanaonekana tu kwa Simba? Na mapungufu hayo hayo hayaonekani wakucheza Yanga au timu nyingine? Sote tumeona muamuzi wa mechi ya Azam na Mtibwa alivyokuwa na mapungufu mengi tu. Ila hakuna anayetoka hadharani na kusema alihongwa tunaambiwa ni mapungufu na makosa ya kibinadamu ila mapungufu hayo hayo yakifanyika kwenye mechi ya Simba mwamuzi anakua amenunuliwa.
Embu tujiulize kosa la Lemere Moro kumrukia mtu kama Van Dame au Brucelee tens akiwa hana mpira na Kosa la Wawa kumchezea rafu Nchimbi lipi lilikuwa kosa kubwa zaidi? Hatukuona watu kulishika bango kosa la Moro na kutaka Tff uchukue hatua. Ila kosa la Wawa ni kama anatakiwa anyongwe au aende jela huu si uungwana.
Kama tumedhamiria kweli kupambana uwanjani kwa haki basi makosa yote yazungumzwe kwa mizania sawa
Nani hakuona Prison walivyonyongwa hasharani pale uwanja wa Uhuru kwa kunyimwa pernat ya wazi huku wao wakipigiwa penat yenye utata. Na ni alitoka hadharani na kupiga kelele kuwa refa kanunuliwa?

Ni Yanga hawa hawa msimu uliopita walipiga kelele mno wakidai Simba inapendelewa kwa kuachwa nyuma kwa viporo ili iwe bingwa. Leo wao ndio wana viporo na wanalalamika pia

YANGA ACHENI KUJIFANYA KAMA WATOTO YATIMA AMBAO HATA MFANYIWE JEMA LIPI MTASINGIZIA MNAONEWA.

NA MBINU ZENU CHAFU ZA KUTAKA KUPATA HURUMA YA MAAMUZI TUMEZISHTUKIA NA SASA INATUFANYA TUONGEZE DOZI ILI KUWAFUMBA MIDOMO KABISA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbinu za Yanga zisikupe shida Mkuu, nakujuza kuwa Simba ndiyo timu pekee imejaza vijana wengi wajanja wa Mjini na wanajua Vigisu zoote za Soka.
Acha wajitekenye na kucheka wenyewe na Viporo vyao vikichacha ndio watajua viporo vinaliwa na ndimu.
 
Back
Top Bottom