Yanga wanaweza kuchukua kombe hili

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Nimeangalia baadhi ya mechi fulani za Shirikisho. Nimegundua Yanga wana timu nzuri, sio kuliko timu zote za shirikisho hapana.

Ila wana baadhi ya wachezaji wazuri kuliko timu zote za Shirikisho. Kinachofanya wachezaji wengi wa Yanga wawe wazuri kuliko timu zote za Shirikisho ni speed ya washambuliaji wao.

Kwa hiyo ni vigumu kucheza na Yanga huku akicheza mpira wa kushambulia na kuacha wachezaji wachache nyuma.

Timu nyingi zinazowafunga Yanga ni zile zinazocheza mpira wa kupaki na kushambulia kwa kushtukiza. Pamoja na zile zinazopata mipira ya kutengwa, maana mabeki wa Yanga ni dhaifu sana kwa mpira ya juu.

Na ninafikiri Kocha wa Yanga ameshalifanyia kazi suala hili. Kwahiyo nawapa Yanga nafasi kubwa ya kuchukua kombe hili.
 
Much appreciated
 
Upo sahihi. Yanga anaweza libeba kama utani

Mazembe na ubovu wake msimu uliopita alifika nusu fainali.

Na amelitwaa hili kombe misimu sio mingi ya nyuma
 
🙌
 
Washambuliaji wenyewe ndo wakina Kithinda ??[emoji23][emoji23]
 
Kwenye mipira ya kutenga bado ni tatizo angalia mechi iliyopita dhidi ya Geita gold
 
Nitarudi kwenye uzi huu baada ya michuano hii kuisha.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Lolote linawezekana .
Ila hatua ya mtoano inakua habar nyingine na uzoefu wa mashindano una matter sna.
Kwa maoni yangu lolote linawezekana maana yanga wamekamilika ,japo kuchukua hili kombe ni process .
Figisu za kibabe zinaanziaga kwenye mtoano .
Swali langu yanga ana uzoefu na figisu za mtoano?
Hili kombe sio km NBC kwamba unaweza jipa uhakika kuwa nabeba .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…