Yanga wanaweza kuchukua kombe hili

Yanga wanaweza kuchukua kombe hili

Sasa mkutane na kilaza kama huyu Gallants halafu mshindwe kupita mtakuwa vilaza kweli. Timu zenye ubora huko ni Pyramid na AS FAR zingine zote ni papatu papatu kama yanga tu.
 
Attachments

  • Screenshot_20230319-231102.png
    Screenshot_20230319-231102.png
    63.1 KB · Views: 4
  • Screenshot_20230319-231024.png
    Screenshot_20230319-231024.png
    36.5 KB · Views: 6
Nimeangalia baadhi ya mechi fulani za Shirikisho. Nimegundua Yanga wana timu nzuri, sio kuliko timu zote za shirikisho hapana.

Ila wana baadhi ya wachezaji wazuri kuliko timu zote za Shirikisho. Kinachofanya wachezaji wengi wa Yanga wawe wazuri kuliko timu zote za Shirikisho ni speed ya washambuliaji wao.

Kwa hiyo ni vigumu kucheza na Yanga huku akicheza mpira wa kushambulia na kuacha wachezaji wachache nyuma.

Timu nyingi zinazowafunga Yanga ni zile zinazocheza mpira wa kupaki na kushambulia kwa kushtukiza. Pamoja na zile zinazopata mipira ya kutengwa, maana mabeki wa Yanga ni dhaifu sana kwa mpira ya juu.

Na ninafikiri Kocha wa Yanga ameshalifanyia kazi suala hili. Kwahiyo nawapa Yanga nafasi kubwa ya kuchukua kombe hili.
Una chembechembe nyingi za kupatia ukweli,hongera tuko pamoja.
 
Lolote linawezekana .
Ila hatua ya mtoano inakua habar nyingine na uzoefu wa mashindano una matter sna.
Kwa maoni yangu lolote linawezekana maana yanga wamekamilika ,japo kuchukua hili kombe ni process .
Figisu za kibabe zinaanziaga kwenye mtoano .
Swali langu yanga ana uzoefu na figisu za mtoano?
Hili kombe sio km NBC kwamba unaweza jipa uhakika kuwa nabeba .
Unaposema figisu ni mentality ya wachezaji na technical bench kwa ujumla mpira wa sasa hivi Africa una mambo mengi nje ya uwanja lakini uwanjani kama uwezo hauna ni hauna tu. Kwa hiyo mpaka kufika hapo uongozi na timu nzima inatambua nini cha kufanya and of course tayari washapata experience ya matatizo wanayoweza kutana nayo(figisu)
 
WAKICHANGA KARATA VYEMA KWENYE ROBO NA WAKATOBOA, ITAKUWA SIMPLE SANA KUIGUSA FINAL.
 
Unaposema figisu ni mentality ya wachezaji na technical bench kwa ujumla mpira wa sasa hivi Africa una mambo mengi nje ya uwanja lakini uwanjani kama uwezo hauna ni hauna tu. Kwa hiyo mpaka kufika hapo uongozi na timu nzima inatambua nini cha kufanya and of course tayari washapata experience ya matatizo wanayoweza kutana nayo(figisu)
Okey acha tuone mtaan
 
Sasa mkutane na kilaza kama huyu Gallants halafu mshindwe kupita mtakuwa vilaza kweli. Timu zenye ubora huko ni Pyramid na AS FAR zingine zote ni papatu papatu kama yanga tu.
Mpira haupo hivyo mkuu, ligi kuu na michuano ya kimataifa ni vitu viwili tofautu. Ac Milan ni timu mbovu hasa kwa kule Italy timu hadi zinazoshuka daraja zina mkazia, lakini kwenye klabu bingwa yupo katika nane bora.
Kwenye CAF champions league msimu huu Kabylie ni timu ya pili kutoka mwisho kwenye ligi ya Algeria lakini kwenye CAF champions league ni timu iliyofuzu akiwa na point kumi sawa sawa na Wydad
IMG_20230320_184517.jpg
IMG_20230320_184544.jpg
 
Ni kweli uko sahihi,kisoka timu zote zitakazofuzu hatua ya robo fainali zinaweza kubeba ndoo ya maji🤣
 
Back
Top Bottom