OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Kabla ya kuanza kwa msimu huu wa mashindano ya CAF, Tanzania ilikuwa katika nafasi ya 13 Afrika, ikiwa na pointi 14.
Pointi hupatikana kwa klabu kuingia hatua ya makundi.
Kwa ligi ya mabingwa, kuingia tu makundi, nchi inapata pointi 2.5, Shirikisho ni pointi 2.
Pointi hizi huhesabiwa kwa kipindi cha miaka 5 na mwaka wa karibu zaidi huwa na thamani zaidi. Kila unapopita mwaka mmoja, pointi moja hupungua kwa kila pointi za mwaka husika.
Tanzania tulizipata pointi zetu kwa mafanikio ya Yanga (2016 na 2018) na Simba (2018/19).
Yanga waliingia makundi Shirikisho na kuipatia Tanzania pointi 2 kila mwaka. Lakini hadi kufikia 2018/19 pale Simba walipoingia robo fainali, pointi za Yanga zilipungua na kubaki 3.
Robo fainali ya Simba iliipatia Tanzania pointi 15, ukichanganya na zile 3 za Yanga, zikawa 18...tukapanda hadi nafasi ya 12 Afrika na kuingiza timu 4 kwenye mashindano ya CAF.
Lakini kukwama kwetu misimu iliyofuata kulitupunguzia pointi. Hadi msimu huu unaanza tukabaki na pointi 14 tu ambazo msimu ujao zitabaki 13.
Lakini Simba kuingia makundi kumetupatia pointi 2 ambazo zinafanya tuwe na pointi 15 msimu ujao.
Hata hivyo, kwenye ligi ya mabingwa, kuingia makundi kuna pointi zake na kila nafasi utakayomaliza kwenye kundi ina pointi zake.
Nafasi ya mwisho ina pointi 5...kwa hiyo Simba hata akiwa wa mwisho kwenye kundi, Tanzania itavuna pointi 5, ukijumlisha na zile 13, zitakuwa 18 msimu ujao.
Wapinzani wetu wakubwa, Libya, ambao walianza msimu wakiwa na pointi 16.5, zitapungua hadi kuwa 13.5 msimu ujao.
Lakini kwa kuwa timu yao ya Al Ahly Benghazi imeingia makundi Shirikisho, msimu ujao Libya itakuwa na pointi 15.5, bado hawatotufikia.
Na endapo Namungo wataingia makundi, wataipatia Tanzania pointi 2, na zile 18, zitakuwa 20.
Ili Libya watuzidi, ni lazima kwanza timu zetu zote ziishie makundi halafu yao ifike hadi robo fainali.
Lakini Simba wakimaliza wa tatu kwenye kundi lao, Tanzania itapata pointi 10, hivyo kuwa na 25....robo fainali, pointi 30.
Na endapo Namungo watafuzu makundi na kumaliza wa tatu...Libya ndo hawatugusi kabisa.
Kutufikia itakuwa ngumu kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
Utopolo wanayajua haya? Kama wanayajua,wanatakiwa kuiombea Simba Sc na Namungo