Yanga wasaini mkataba wa milioni 900 na Shirika la Bima la Taifa (NIC)

Franky Samuel

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2018
Posts
5,195
Reaction score
13,785
"Kihistoria taasisi hii ya Bima ya Taifa ndio taasisi kongwe kabisa kutoka serikalini ambayo imeanzisha miaka 60 iliyopita. Ni heshima kwetu kuingia kwenye mkataba wa utoaji wa zawadi ya mchezaji bora wa mwezi wa Young Africans SC na taasisi hii yenye heshima kubwa kwa taifa" Rais wa Young Africans SC @Caamil8
"Makubaliano haya ya kibiashara kimsingi yanakwenda kunufaisha pande zote. Young Africans SC inakwenda kupata kiasi cha 𝐓𝐬𝐑 πŸ—πŸŽπŸŽπ¦ kwa kipindi cha miaka mitatu. Vile vile kutangaza biashara ya BIMA. Wananchi, BIMA ni NIC pekee" @Caamil8
"Tunaelewa kwanini Shirika la BIMA la TAIFA limechagua kufanya kazi na sisi. Tuna Wachezaji bora zaidi ambao huwezi kuwapata kwenye Klabu nyingine. Wachezaji hawa wana ushawishi mkubwa nje na ndani ya Uwanja. Ushawishi wao ni chachu ya kutangaza biashara hii ya BIMA" @Caamil8
"Tunawahakikishia Shirika la Bima la Taifa kuwa tutakuwa na ushirikiano mzuri sana katika kuhakikisha matakwa haya ya kimkataba yanatekelezwa kwa weledi mkubwa" @Caamil8
"Mkataba wa Shirika la BIMA la Taifa (NIC) limechagua taasisi kubwa ambayo inaweza kuendana na maana ya ukubwa. Sisi ni wakubwa tunafanya kazi na wakubwa wenzetu. Kila mwananchi anapaswa kujua BIMA ni NIC tu. Young Africans ni timu ya Kidigital na NIC ni BIMA ya kidigital zaidi" Karim Meshack - Mkurugenzi Masoko NIC
"Tunafurahi sana kuingia mkataba na NIC kwa sababu kutakuwa na ushindani mkubwa kwa Wachezaji wetu. Hamasa itakuwa kubwa kutoka kwa mashabiki wetu. Bila shaka michezo yetu watakao trend mitandaoni baada ya mechi ni wachezaji tu na sio mtu mwingine. Kuna wengine wakimaliza mechi malalamiko yanakuwa makubwa mitandaoni kuliko Wachezaji wao kutrend" @AliKamwe
Leo historia imeandikwa baada ya taasisi mbili zenye chapa ya kihistoria kwa Tanzania kuingia makubaliano ya kibiashara kwa miaka mitatu. Huwezi kuzungumzia BIMA kama huitaji NIC, na katika soka Young Africans ndio nembo ya soka kwa Tanzania" Elihuruma Doriye - Mtendaji Mkuu - NIC
 
Hapo pia kuna milioni 900 ya Simba
 
β€œLeo Yanga SC imeingia mkataba ghali na wa kihistoria na NIC wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi. Huu ndio mkataba ghali zaidi wenye thamani ya Milion 900 kwenye Tuzo za mchezaji bora wa mwezi” Ally Kamwe
 
Naunga mkono hoja πŸ‘πŸ‘
 
β€œLeo Yanga SC imeingia mkataba ghali na wa kihistoria na NIC wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi. Huu ndio mkataba ghali zaidi wenye thamani ya Milion 900 kwenye Tuzo za mchezaji bora wa mwezi” Ally Kamwe
Yanga sc tuna watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…