Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Klabu ya Yanga inahusishwa kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Azam fc Prince Dube baada ya mchezaji huyo kumalizana rasmi na timu hiyo lakini hapo awali kulikuwa na tetesi nyingi sana kumuhusu Dube kujiunga na Yanga lakini pia Simba.
Mimi naomba nishare nanyi kidogo kwa kile ninachokiona kwenye ishu hii ya Dube na Yanga
1. Dube ni mchezaji mzuri katika eneo lake la ushambuliaji
2. Anauwezo wa kufunga kama tulivyomshuhudia akiwa na Azam kwa misimu kadhaa akifanikiwa kufunga zaidi goli 10 kila msimu kwenye ligi
3. Anauwezo wa kutulia katika eneo lake la mwisho na kutumia ubunifu mkubwa katika kufunga.
La kuzingatia sasa kwa Yanga ni hili licha ya ubora wote wa Dube, lakini anachangamoto moja kubwa ya kupata majeruhi kila msimu na kumfanya kukaa nje ya uwanja kwa muda kidogo, sasa ukizingatia Yanga wapo katika ushindani mkubwa katika mashindano yote wanayoshiriki katika msimu mzima kwahiyo wakitegemea Dube awe top mshambuliaji, huko mbele wanauwezo wa kukwama tena katika michezo muhimu zaidi.
Yanga wanapaswa kufanya usajili wa mshambuliaji Kinara ambaye backup yake ndiyo inaweza kuwa huyo Dube kama ilivyokuwa kwa Mayele wakati akiwa Yanga backup yake alikuwa nayo kama wakina mzize na wengineo.
Kwahiyo Yanga watazame hapo ili baadae wasije wakajilaumu na Dube atambue kwamba huku atakutana na ushindani mkubwa zaidi kuliko alivyokuwa Azam fc kwahiyo ikitokea amesajiliwa ajuwe kabisa atakuwa anawakati mkubwa wa ushindani zaidi.