Yanga watalazimika kumpigia magoti mzee Akilimali? Yanga wanaweza bila mzee Akilimali?

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaam wana jamvi.
Baada ya Yanga kulazimika kumpigia magoti Manji baada ya Mzee Akilimali kupingana na pendekezo lake kutaka kuikodi Yanga kama movie za kutazama.

Wana jamvi bila shaka wafatiliaji wa soka mtakuwa mna mfahamu vyema huyu mzee.. Huyu mzee akiwa amenuna au kuchukia timu haiwezi kupata mafanikio maana wadadisi wanasema huyu mzee ndio anajua Yanga ilipo na ndio mwenye Yanga na hata wanachama wa Yanga wanajua huyu ndiye mwenye Yanga.

Hata Yusuphu Manji anajua kabisa Akilimali ndio anajua Yanga ilipo na ilipo wekwa..
Sasa badaada ya Yanga kumsimamisha uanachama na kupendekeza mkutano mkuu umfute uanachama Akilimali ni wazi kabisa kuna siku Yanga watalazimika kumrudisha na kumuomba msamaha mzee Akilimali kama walivyo fanya kwa Yusuphu Manji.

Yanga hawana uwezo wa kusimama bila huyu Mzee hata wao wanajua. Na kumbuka kuna kipindi waligombana nae akasema kuwa watamkubuka na ilikuwa wanaelekea kwenye pambano lao na Simba lakini kilicho wapata Yanga wanajua na walilazimika kumuomba radhi..

Jana Yanga wamemsimamisha mzee Akilimali uanachama leo hii wamepewa zawadi na Azam..

Huyu mzee hana pesa ila anajua Yanga ilipo kwa hiyo hata Manji bila shaka hatokubali mzee huyu afukuzwe maana anajua fika huyu ndio anajua Yanga ilipo..

Hakika Mzee Akilimali anajua Yanga ilipo..

Karibuni wana jamvi.
 
 
karne hii eti wazee hivi OLIMPIC TUTAFIKA KWELI?HIVI LEO UNAMWAMBIA BOLT ILI USHINDE LAZIMA MZEE AWEPO NASEMA HIV AFRICA TUNATATIZO TRUMP HAKUKOSEA SISI BADO SANA
 
karne hii eti wazee hivi OLIMPIC TUTAFIKA KWELI?HIVI LEO UNAMWAMBIA BOLT ILI USHINDE LAZIMA MZEE AWEPO NASEMA HIV AFRICA TUNATATIZO TRUMP HAKUKOSEA SISI BADO SANA
Mkuu pale Arsenal, Manchester United hakuna wazee? haha Bongo kwenye nyosoo
 
Kijiji hakikosi wazee bhana hiyo ni laana ya akilimali
 
karne hii eti wazee hivi OLIMPIC TUTAFIKA KWELI?HIVI LEO UNAMWAMBIA BOLT ILI USHINDE LAZIMA MZEE AWEPO NASEMA HIV AFRICA TUNATATIZO TRUMP HAKUKOSEA SISI BADO SANA
Mkuu wala hatufiki kabisa kabisa.....
 
Inasikitisha sana brand name kama Young Africa, bara zima la Africa inatambua timu hii, big name and goodwill lakini waTanzania kwa maelfu wanahojiwa na kuongea upuuzi mwingi mara akilimali, mara manji, nimeamini Tanzania kuna wapumbavu wengi sana na wanastahili vifungo cha maisha. Nikiangalia TV na kusikiliza radio mijitu yote inamlilia manji, hvi kweli club kubwa kama yanga inahitaji upuuzi huo??? Leo hii kila mwanachama wa yanga Tanzania akanunua hisa moja kwa Tsh 500/=, bado mtamnyenyekea mdosi manji????? Watanzania acheni ujinga nyinyi.
 
Kwani Azam hajawahi kumfunga Yanga na huuo Mzee Akilimali akiwepo ?
 
Laana ya kutukana Wazee itaitafuna Yanga mpaka wawapigie magoti
 

....idea yako kwa kuifikiria inaonekana rahisi sana!, ila ipeleke kwenye implementation ndio utaona ugumu wake, siku zote kinachorudisha nyuma hivi vilabu vikubwa ni Uongozi mbovu,viongozi hawana dhamira za dhati kuvisogeza mbele hivi vilabu, zaidi ya kuvigeuza shamba la bibi!

.....patatakiwa pawepo na namna ya kusimamia mapato yatakayopatikana kutokana na mauzo ya hizo hisa,na adhabu kali itolewe kwa kiongozi atakayethibitika kuhujumu mapato hayo, kwa namna yoyote,tukiweza kusimamia hili, hizi timu zitakuwa unstoppable Africa!

...kwasababu sisi wenyewe tumeshindwa kulisimamia hilo,ndio sababu hawa wafanyabiashara wameamua kuja kuwekeza kwenye hizi timu, kwa kuiona fursa iliyopo,binafsi wala siwalaumu,ni haki yao, sababu uwezo wanao na opportunities km hizi ndio kitu mfanyabiashara anakitazama siku zote.

....mpaka tutakapo kuwa tayari ndio tuvirudishe hivi vilabu mikononi mwa wanachama,ni muhimu hawa watu wapewe hizi timu kwa mkataba,km ni miaka mitatu au minne wawe wana renew,siku akili za wanachama zitakapoamka, ndio tuvirudishe mikononi mwetu, kwa kufanya niliyoandika hapo juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…