Smart codetz
JF-Expert Member
- Jan 25, 2023
- 218
- 875
YANGA imeeleza sababu ya winga wake Bernard Morrison 'BM33' kutotumika kwenye mchezo wa kwanza robo fainali Kombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United uliopigwa kwenye Uwanja wa Godswill Akpabi nchini Nigeria.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Yanga kupitia kwa Kocha msaidizi Cedric Kaze amefichua kuwa sababu iliyofanya benchi la ufundi kutomtumia winga Morrison kwenye mchezo huo ni kupata majeraha.
Morrison alipata shida kidogo ya msuli kwenye mazoezi ya mwisho hapa Nigeria, kama benchi la ufundi tukaona sio sawa kumlazimisha acheze kwani anaweza kuumia zaidi" amesema Kaze