Yanga Ya Lwandamina yachezea kichapo vs JKU

Yanga Ya Lwandamina yachezea kichapo vs JKU

Mkuu ile kazi iliyokua ikinipeleka eneo korofi nilishaimaliza.. Hivyo sitegemei kurudi tena huko.
Tusubiri mechi mbili tu za mwanzo. Mtaanza kusema Mkude na Ajib wanahujumu.
 
Kwani bado hawajasaini Yanga?Si ilikuwa wananukia kusajili Yanga?Au harufu imepotea?
 
Leo vipi...? Mmeshinda?.... [emoji23][emoji23][emoji23]
 
SIMBA YA OMOG YAPIGWA RISASI MBILI ZA TAKONI
Wanamghana wao wanamwita circuit breaker mungu si athuman jana mida ya saa kumi circuit breaker ika trip mbaka wanampata fundi wa kufanya tracing saa mbili usiku
 
Sisi hata mazoezi tunashindaga

SAFARI BADOOOOOOO!!!

Baada ya watani zao Yanga kufungwa magoli 2-0 dhidi ya JKU ya Zanzibar mchezo wa Kirafiki na jioni ya Leo timu ya Simba imepokea kichapo cha magoli 2-1 toka kwa Mtibwa Sugar mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex,Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Mchezo huo ulikuwa kwa ajili ya kusherekea Maulid Day na Simba walikuwa wakiwajaribu wachezaji wao wapya toka nchini Ghana kipa Daniel Agyei na kiungo mkabaji James Kotei dakika ya kwanza Stahmili Mbonde aliifungia Mtibwa goli la mapema.
Vijana wa Joseph Omog walijaribu kusawazishi hata hivyo Jaffari Salum aliwanyanyua mashabiki wa Mtibwa dakika ya 34 na dakika ya 36 kiungo wa zamani wa Mtibwa Ibrahim Mohamed aliifungia Simba goli hadi mapumziko Mtibwa walikwenda wakiwa kifua mbele kwa magoli mawili.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyo Simba watajilaum wenyewe baada ya kupata penati iliyopigwa na Janvier Bokungu dakika ya 88 na shuti lake liligonga mwamba hadi mpira unamalizika Mtibwa wameibuka na ushindi wa magoli 2-1.


Mchezo huu ulikuwa wa pili kwa Simba mchezo wa kwanza walishinda magoli 2-0 dhidi ya Polisi Moro inayoshiriki ligi daraja la kwanza wakati nao Mtibwa ulikuwa wa pili baada ya kucheza na Azam FC na kutoka sare ya 2-2 ikiwa ni michezo ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inayotarajiwa kuanza Desemba 17,mwisho wa juma hili.

VIKOSI:Simba: Daniel Agyei, Jenvier Bukungu, Mohammed Hussein, Novaty Lufunga/Abdi Banda dk46, Method Mwanjali, James Kotei/Muzamil dk73, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Jamal Mnyate dk84, Fredrick Blagnoon/Laudit Mavugo dk70, Mussa Ndusha/Ibrahim Hajib dk60 na Mohammed Ibrahim.
Mtibwa Sugar: Said Nduda, Ally Shomary, Hassan Timbe, Henry Joseph, Salim Mbonde, Shaban Nditi, Kelvin Friday, Mohamed Banka, Stamili Mbonde, Jafary Salum/Mandawa dk73 na Haruna Chanongo/Vincent Baranabas dk76.


Source: SIMBA KAMA YANGA,YANYUKWA NA MTIBWA SUGAR CHAMAZI - Full Shangwe Blog
 
Back
Top Bottom