Yanga ya moto sana!

Daniel Mwinula

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2012
Posts
302
Reaction score
328
Binafsi, pamoja na kuwa ni shabiki wa Yanga, naomba nipongeze uongozi kwa ku-maintain ubora wa timu.

Jaribio la jana, kiukweli lilikuwa ni jaribio KUBWA sana lililokuja MAPEMA sana, lakini bado pamoja na jaribio kuja mapema wakati bado kocha mpya na wachezaji wapya hawajazoeana sana TULIFANIKIWA KULIWEZA.

Kwa mpira ule, binafsi natabiri makubwa sana kwenye ligi yetu.
 
Kikubwa yule Skudu aache kucheza na jukwaa,na Mzinze anazingua
 
Bila BAHASHA hesabu maumivu
 
Mimi kama mimi, nimeanza eti kuiogopa hii timu! 🤔

Hivi kocha wa Makolo anaweza kweli kuchezesha vikosi viwili ndani ya dakika 90 kama alivyofanya kocha wa Yanga!! Au atawaogopa wale mashabiki kasuku wanaotaka Chama acheze kwenye kila mechi, na kwa dakika zote!!
 
Mimi pia kitendo alichokifanya coach kilinistua, ingawa ndiyo maana halisi ya kutafuta kikosi.
 
Mimi pia kitendo alichokifanya coach kilinistua, ingawa ndiyo maana halisi ya kutafuta kikosi.
Lakini hii si ndio inakuwaga utaratibu wa Yanga kwenye mechi zote za siku ya wananchi? Kama kumbukumbu zangu zipo sawa nadhani ni miaka yote inakuaga hivyo vikosi viwili vinachezeshwa. Tofauti na upande wa pili wao wanajali zaidi matokeo hivyo sub huwa wanafanya za kiufundi zaidi hivyo key players huwa hawawatoi labda kama kuna mtaji wa magoli. Ila kwa Yanga wiki ya mwananchi kama sehemu tu ya burudani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…