Yanga: Yaaani tuuze mechi milioni 8?

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
YANGA imedai kwamba iligoma kuuza haki za matangazo ya Televisheni za mechi yao na BDF XI ya Botswana kwa vile Azam
TV haikufika dau.

Katibu wa Yanga, Jonas Tiboroha, ameweka wazi kwamba mechi zao wanaanza kuuza kwa dau la dola 10,000 (Sh 18 milioni) dau ambalo hakuna chombo chochote nchini kilichoweza kulifikia.

"Tulikuwa na mazungumzo na baadhi ya TV, lakini hawakuweza kufika kiwango chetu tukakacha biashara hiyo kwani haikuwa na manufaa kwetu, hivyo tukaona bora kusubiri mapato ya mlangoni," alisema kiongozi huyo mwenye uelewa wa mambo ya ufundi wa soka uwanjani.

Alitolea mfano wa tathimini ndogo waliyofanya kwamba waligundua kuwa kitendo cha kuonyesha mechi kinapunguza watu kwenda uwanjani kuangalia mchezo hivyo kupunguza pato.

Alifafanua kwamba kama Azam TV wangeonyesha mechi hiyo, kampuni mama ya kituo hicho ingefaidika mara mbili kwani matangazo ya biashara zake za unga, juisi na lambalamba yangeonekana mbali na kuzidi kupata wateja huku Yanga ikiambulia kidogo.

"Mlango upo wazi kwa TV inayotaka kuonyesha mechi zetu, lakini kwa kuzingatia dau linalotakiwa kulingana na uzito wa mechi," alisema na kudai kwamba Azam iliweka Sh8 milioni mezani ambazo ni kiduchu. Tiboroha alisema soka ni biashara, hivyo lazima wazingatie masuala ya uchumi ambayo ndio misingi ya kuleta maendeleo ya kufika mbali.

MwanaSpoti
 
Viongozi wa Yanga ni wabinafsi, wanajifikiria wao na washabiki wao wa Dar es Salaam wenye uwezo wa kufika uwanjani. Wao wana VIP tiketi za bure, na hata kama wasingekuwa nazo wana uhakika wa kuingia uwanjani lakini hawafikiriii kuna washabiki wao walio nje ya jiji.

Na hata waliopo ndani ya jiji wakija wote uwanja hautoshi.

Hoja ya kuwa wakionesha washabiki hawatakuja ni hoja dhaifu sana, Kombe la Dunia huoneshwa duniani kote na bado watu hujaa viwanjani.

Hoja ya msingi: Hawa jamaa hawana usiri wa biashara? Kwanini uanike kwa waandishi kila mlichozungumza na washirika wenu wa biashara, inatia shaka kwa mtu ambaye anataka kufanya kazi na ninyi kesho!

Nilikuwepo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…