Yanga yaachana na Mkurugenzi wa Ufundi, Hans Pluijm

Jikumbusheni story ya Chuji kuhusu tano bila aliyopigwa yanga na simba tatizo lilikuwa ni pesa hivyohivyo
 
wapi Akilimali na wenziwe? mbaya wenu Manji ndiyo hivyo tena...sasa ni wakati wenu wa kuonyesha ule msuli wenu mliokuwa mnamtunishia Manji wakati ule!
 
Huyu kocha akienda azam ndo safi namkubali Sana anajua haswa
 
wapi Akilimali na wenziwe? mbaya wenu Manji ndiyo hivyo tena...sasa ni wakati wenu wa kuonyesha ule msuli wenu mliokuwa mnamtunishia Manji wakati ule!
Yanga,a.k.a chura mna matatizo sana
 
Team inashuka daraja hiyo kila mtu pale kwa hari hii ataonekana mzigo tu hela ndio inapanga
 
hahahaha Yanga hela hawana halafu walikurupuka kumvua huyu pujin ukocha hakika watajuta.......
 
Pamoja na kuwa Pluim ni kocha mzuri,bajeti kubwa pale Yanga ilikuwa inambeba. Kila mchezaji anayemtaka anakuja. Wakibattle kugombea mchezaji na Simba,Simba hapindui.

Ila kwa swala la Record Lwandamina yuko Juu zaidi ya Pluim. Yeye Lwandamina kaifikisha Zesco (inamilikiwa na Shilika la umeme Zambia) nusu finali ya klabu bingwa Africa 2016. Wakati babu kaishia makundi ya kombe la shirikisho tena kashika mkia.
 
Chanzo namba 1 cha mapato kwa timu kiingilio,tatizo la timu zetu ni bajeti kubwa kuliko mapato hasa kwenye mishahara
 
Plujim licha ya kupata mafanikio aliongeza viwango binafsi kwa wachezaji kama Simon Msuva,Juma Abdul,Haji MwinyiObren Chirwa,Deus Kaseke,Deo Munishi,Amis Tambwe.

Kuipeleka timu nusu fainali inategemea aliikuta timu kwenye level gani,Plujim ameikuta Yanga ikiwa wasindikizaji kwenye michuano ya kimataifa na kwa misimu 2 tu alishaibadilisha timu naamini msimu huu angeweza kuifikisha Yanga nusu fainali
 
Poleni sana watani,mnapoteza jembe kwa ajili ya ukata
 
ALIKATAA KYONGOZANA NA MASHABIKI KWENDA KUMUANGALIA MANJI WAKATI AKIWA SERO..HII KWA KWELI IMETUUZI SANA HIVYO LAZIMA ATIMULIWE

Hivi katika contract yake pamoja na schedule of duties kulikuwa na kipengele cha kuandamana na mashabiki kwenda kumwangalia Manji mahabusu?? Huu ni ujinga uliopitiliza
 
Bajeti ya timu izungumzie.
Tambwe kaongezewa nini?
Yanga ni Ngoma na Kamusoko.

Timu chini yake msimu huu ilizidiwa 8 points.

Zesco kabla ya Lwandamina ilifika level gani? Kakaa nayo si chini ya 2 years.
 
Yanga na badooo mpaka mnyooke mmezoea mteremko mnooo!
 
Bajeti ya timu izungumzie.
Tambwe kaongezewa nini?
Yanga ni Ngoma na Kamusoko.

Timu chini yake msimu huu ilizidiwa 8 points.

Zesco kabla ya Lwandamina ilifika level gani? Kakaa nayo si chini ya 2 years.
Mpira sio rahisi kama unavyoandika

1.Assessment ya timu hufanywa baada ya msimu,yaani ulitaka Yanga iongoze ligi kuanzia mechi ya kwanza hadi ya mwisho,hii uliwahi kuona wapi ?

2.Huwezi pata mafanikio ya kimataifa bila kufanya vizuri michuano ya ndani na Plujim alifanya vizuri misimu 2 ndani na timu ilianza kufanya vizuri michuano ya kimataifa na ilikuwa inacheza vizuri,mara ya mwisho Yanga kufika hiyo stage ni 1998

3.Unajua Msimu ujao Yanga wanaweza wasicheze hata michuano ambayo unamsifia Lwandamina alifanya vizuri huko Zesco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…