Yanga yafungiwa na FIFA kufanya usajili kwa misimu 3

Yanga yafungiwa na FIFA kufanya usajili kwa misimu 3

Hata yanga hii kesi wakili wa Tambwe amesema yanga nao walikata rufaa CAS wakashindwa

Yanga baada ya kushindwa ndo adhabu hiyo wamepewa walipe pesa ya Tambwe au wakakutane na hicho kifungo
 
Ebu nikumbushe kidogo kuhusu Barcelona na Chelsea waliishawahi kukutana na adhabu kama hizi ila makosa tofauti je hizo adhabu ziliishia wapi?
Mfano chelsea aliwahi kukata rufaa na kushinda ila Yanga ameshakata rufaa CAS na ameshindwa hivyo alitakiwa kumlipa Tambwe hata hivyo hawakufanya hivyo ndio maana Fifa ikafikia maamuzi hayo
 
Kwahiyo unataka kuniambia Yanga wanashindwa kulipa hilo deni au ni dharau tu za viongozi waliopo madarakani
Dharau tu Mkuu, maana kuna wengi wanawadai wanapenda kuvimbia mamlaka pasi na sababu

Hivi suala la kulipa pesa za mchezaji tena anastahili swala la kupinga au kukata rufaa
 
Amiss Tambwe ni Team Yanga yule! Hawezi kamwe kuiumiza timu ambayo alitamani mara kadhaa kuja kumuona mwanaye aliyezaa na yule mke wake wa Kitanzania anakuja kuichezea siku moja!

Timu ya Wananchi. Mbumbumbu fc muwe mnajiridhisha kwanza kabla ya kuja na taarifa feki za kulishwa na viongozi wenu wababaishaji.
 
LIPENI HELA WAJINGA NYIE BADO ZAHERA,DANTE, KESSY ,YONDANI,.MTASAJILI 2024..POLENI MANYANI FC
Hata Yanga isajili 2024, bado itaendelea kubakia kuwa moja ya timu bora kabisa. Ina wachezaji lukuki vijana tofauti na timu yenu iliyojaa wazee!!

By the way, ile mil.300 ya Kichuya mlishalipa? Au bado mnaendelea kumlamba miguu Mwamedi ili awalipie?
 
Bongo hamna waandishi wa habari Bali Kuna waandishi wa udaku

Nimemsikiliza huyo wakili wa tambwe, anasema "Yanga waliambiwa wamlipe tambwe, Yanga wakaenda CAS kupinga adhabu, Yanga wakashindwa tena, Jana huyo wakili kapewa taarifa kwamba Yanga wamefungiwa kusajli madirisha 3 mpaka pale watakapo lipa kifungo kinaisha, na Kama hawato lipa kabsa basi wanakatwa points na rungu kubwa zaidi"

Sijaona Cha ajabu hapo waandshi kushikiria bango. Maana Yanga SC watalipa tu.

Week iliyopita meneja wa zaman wa Simba SC nae alikuwa na matatzo Kama hayo, ila waandishi hawajashadadia, sijui kwa sababu ni mbongo
Swala la Tambwe na la meneja wa zamani ni tofauti ingawa wote wana madai, meneja wa zamani wa simba swala lake liko mahakama ya kazi kitengo cha usuluhishi wakati swala la Tambwe lilishatolewa maamuzi lakini yanga wamegoma kutekeleza.
 
Taarifa ni ya kweli bro,wachezaji na makocha wa misimu ya2017, 2018-19 timu ilipokua na wapigaji kina nyika wengiwao walikua wanadai,kuna waliolipwa na wanaoendelea kulipwa baada ya kuingia uongozi wa kina msola,tambwe atalipwa pesa yake na Yanga itaendelea kusajili kama kawaida,manta hofu
Sawa, nimeshathibitisha

Hili nalo litapita
 
Amiss Tambwe ni Team Yanga yule! Hawezi kamwe kuiumiza timu ambayo alitamani mara kadhaa kuja kumuona mwanaye aliyezaa na yule mke wake wa Kitanzania anakuja kuichezea siku moja!

Timu ya Wananchi. Mbumbumbu fc muwe mnajiridhisha kwanza kabla ya kuja na taarifa feki za kulishwa na viongozi wenu wababaishaji.
Tuliza mshono, Amisi Tambwe hakuja kutangaza dini hapa alikuja kufanya kazi ili apate fedha. Huyo mtoto mwenyewe hadi sasa ana mababa zaidi ya watano.
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani, FIFA imefikia uamuzi wa Kuifungia Timu ya Yanga baada ya kushindwa kumlipa Hamisi Tambwe malimbikizo ya mshahara na pesa za uhamisho kiasi cha Jumla Tsh Millioni 44.

Na sasa Yanga Haitaweza kufanya usajili kwa muda wa miaka mitatu kuanzia sasa.

Poleni Sana Yanga, Baada Ya Bumbuli Sasa Mnakutana Na Rungu la FIFA poleni.
Dalali wa magodoro anasemaje kwani, au usanii usanii tu?.
 
Sijaelewa sasa hapo hao fifa wamemsaidia vipi tambwe?
Wameamsaidia vipi?!!hapo lazima pesa yake alipwe!!muwe mnaelewa, hiyo ni hatua ya mwanzo, muda ukipita hajalipwa adhabu nyingine itafuata, na kama mtakuwa wagumu inakuja nyingine(kushushwa daraja)mkiendelea kuwa wagumu tena mnafutwa kabisa katika ulimwengu wa soka!!lakini haki yake italipwa tu hata mkihamia kwenye mchezo wa DHUMUNA!!
 
Back
Top Bottom