Yanga yajitoa Michuano ya Kombe la Kagame mwaka huu

Yanga yajitoa Michuano ya Kombe la Kagame mwaka huu

Queen V

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2012
Posts
775
Reaction score
1,332
236a3586-ebaa-41a5-8835-c6ee94cae0f7.jpg

Timu ya Soka ya Young Africans “Yanga” imetoa taarifa ya kutoshiriki Kagame Cup mwaka 2019 kutokana na changamoto mbalimbali.

Changamoto zilizotajwa ni pamoja na

1. Wachezaji wengi kumaliza mkataba

2. Wachezaji wachache wenye mikataba walisharuhusiwa kwenda kwenye mapumziko ya mwisho wa msimu.

3. Baadhi ya wachezaji na mwalimu watakuwa kwenye ushiriki wa AFCON nchini Misri.

4. Wachezaji ambao timu ipo kwenye taratibu za kuwasajili bado hawajamaliza taratibu za mwisho kwenye vilabu vyao.
 
Waliomaliza mikataba ni akina Matheo, Mahadhi, Ngassa, Makapu, Kabwili, Juma Abduli, Tambwe, Kamusoko,Ajibu, Kindoki wengine ni wapi?
 
Musonye amekosa jipya atoke. Kiongozi gani upo toka enzi niko primary mpaka leo halafu uwe na kipya? Mashindano yalitakiwa yamefanyike hata kila baada ya miaka miwili. Na kuepuka ratiba kuingiliana
 
Musonye amekosa jipya atoke. Kiongozi gani upo toka enzi niko primary mpaka leo halafu uwe na kipya? Mashindano yalitakiwa yamefanyike hata kila baada ya miaka miwili. Na kuepuka ratiba kuingiliana

Zamani timu yenu Simba na yetu Yanga tulikua tunayapenda kwa kuwa tulikua hatujaonja utamu wa CAF tournaments, ila toka tumeonja hatutaki tena na ni kweli ratiba ya ligi yetu si rafiki
 
KAGAME CUP mwaka huu watakosa mvuto, sijui hata Azam kama watairusha kwenye TV,heri waalike timu ndogo kama mtibwa,na kina KMC
 
Mshindano mazuri ila mpangilio ndio mbovu. Mashindano haya yangekuwa yanazisaidia sana timu za ukanda kama yangekuwa yanaandaliwa vizuri na yana ratiba nzuri
 
Hawa Cecafa wajinga sana,wamepeleka mashindano Rwanda cos haijafuzu Afcon, halafu wanafanya mambo kizamani sana,ilatakiwa haya mashindano yaingizwe kwenye ratiba ya mashirikisho na hata Caf na Fifa lasivyo Musonyi atakuwa anapoteza muda tu
 
Mikataba...Mikataba, mwaka jana sababu kama hii ilitolewa.

Ngoja tusubiri mwaka ambao ukiisha msimu wachezaji nao mikataba haitaisha.
 
Waliomaliza mikataba ni akina Matheo, Mahadhi, Ngassa, Makapu, Kabwili, Juma Abduli, Tambwe, Kamusoko,Ajibu, Kindoki wengine ni wapi?
Mkuu yanga kwa wachezaji waliocheza last season wanabaki watano tu,Tshishimbi,Gadiel,Yondani,Feisal na Paul Godfrey.........Timu inatengenezwa mpya kabisa chini ya Mwinyi Zahera
 
Hizo tetesi we umezipata wapi,mbona kama ni hivo wachezaji wengi wataachwa aisee na wataenda wapi,duh
Mkuu yanga kwa wachezaji waliocheza last season wanabaki watano tu,Tshishimbi,Gadiel,Yondani,Feisal na Paul Godfrey.........Timu inatengenezwa mpya kabisa chini ya Mwinyi Zahera
 
Zamani timu yenu Simba na yetu Yanga tulikua tunayapenda kwa kuwa tulikua hatujaonja utamu wa CAF tournaments, ila toka tumeonja hatutaki tena na ni kweli ratiba ya ligi yetu si rafiki
Kweli kabisa! Mashindano ya CACL mazuri Sana hata haya Cecafa hayana msisimko inabidii wajipange waje kivingine.
 
Hizo tetesi we umezipata wapi,mbona kama ni hivo wachezaji wengi wataachwa aisee na wataenda wapi,duh
Mkuu we subilia utaona mwisho wake utakuwaje,staki kusema nimetoa wapi ila hiyo ni taarifa ninayokupa ipokee na subiria confirmation yake baadaye
 
Back
Top Bottom