MICHEZO
UPUMBAVU WA NICHOLAS MUSONYE
Hakika ni muda mrefu sana klabu ya Yanga imekuwa haizungumzwi vizuri na Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye, zipo sababu anazojua yeye Musonye chuki hizo dhidi ya Yanga.
Ni dhahiri shahiri kuwa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, timu za Yanga na Simba ndizo timu zenye washabiki wengi sana, timu hizi si kwamba zina washabiki ndani ya nchi ya Tanzania tu, bali hata kwenye nchi za jirani za Kenya, Uganda, Zambia, Burundi na hata Rwanda, vilabu hivi vina washabiki na wapenzi wengi sana.
Mashindano yoyote yale yatakayoandaliwa kwa sura ya Afrika Mashariki na kati, panapokosekana timu za Yanga na Simba basi ladha ya michuano hiyo hupotea, hapa ndipo panapomfanya Nicholas Musonye kuwehuka kwa dhana ya kupooza michuano hiyo.
CECAFA hivi karibuni ilitoa mualiko wa kushiriki michuano ya klabu bingwa ya Afrika mashariki na kati yatakayofanyika siku zijazo huko nchini Rwanda, pamoja na mualiko huo, klabu ya Yanga haikuwahi kujibu kuwa itashiriki ama haitoshiriki michuano hiyo.
Klabu ya Yanga baada ya kutafakari kwa makini faida za ushiriki wa michuano hiyo, ilifikia kuandika barua iliyotanabahisha kuwa haitoshiriki kwenye michuano hiyo kwa sababu walizozitoa, yumkini sababu walizotoa ni za msingi sana, maana ni kweli Yanga inafanya usajili mkubwa sana, kiasi cha kuibadilisha karibu timu yote kwa ujumla, wapo wachezaji ambao wamemaliza mikataba, pia hata wale wanaoendelea na mikataba walishapewa likizo za mapumziko, karibu nusu ya wachezaji ni wapya, hivyo taratibu za usajili bado hazijakamilika na si haki kumchezesha mchezaji asiyekamilika kiutaratibu za usajili, wapo wachezaji waandamizi kwenye timu za taifa zinazoshiriki michuano ya AFCON huko nchini Misri,
Kimsingi sababu zilizotolewa na uongozi wa Yanga zina tija sana.
Nicholas Musonye amepaniki sana baada ya kupata taarifa ya klabu ya Yanga kuamua kutoshiriki michuano hiyo, amefikia kutoa maneno machafu dhidi ya klabu yetu ya Yanga, kiujumla wanayanga tumechukizwa na kauli za Musonye, hivyo basi nasi tunamjibu kama ifuatavyo:-
Kwanza Musonye ni Mpumbavu sana, si kiongozi mwenye sifa za uongozi wa soka, nadiriki kumwambia kuwa yeye ndiye chanzo kikuu cha kuzorota soka kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
Musonye hajui kupanga kalenda itakayokuwa rafiki na kalenda za FIFA, CAF na Mashirikisho ya vyama vya soka ambavyo ni wanachama wa CECAFA.
Musonye ni mtu mwenye tamaa ya pesa zaidi kuliko maendeleo ya soka, ndio maana ilifikia kuzipanga kwenye kundi moja mechi ya Yanga na Simba, kusudi lake hajikusanyie mapato ya haraka haraka.
Musonye tambua kuwa Yanga sio wajinga ama wapumbavu kama wewe, Yanga ni klabu iliyoanzishwa kabla ya hata baba yako hajazaliwa, hivyo unalazimika kuiheshimu sana, maana imekuzidi umri sana.
Musonye elewa kuwa wewe kung'ang'ania kwako ukatibu wa CECAFA ndio chanzo cha kuiuwa hiyo CECAFA, maana muda si mrefu itaitwa SI KAFA.
Musonye kwani lazima huwe katibu wa CECAFA milele, je huwezi kufanya kazi zingine? huko Kenya haswa jiji la Mombasa zipo kazi zitakazokufaa na kuziweza sana.
Musonye fahamu kuwa tumekuchoka kwa maneno yako ya kashfa dhidi ya klabu yetu kongwe kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
Leo naishia hapa, japokuwa yapo yaliyo mengi tumekuwekea akiba, pindi ukiendelea kuisema vibaya klabu yetu ya Yanga. Aidha kama ujumbe uliosomeka mitandaoni si wako, basi andiko hili litafutika rasmi.
YANGA OYEE.
M.S.B
Mzingwi Mpole
2019.